TANGAZO


Sunday, April 27, 2014

Bondia Thomas Mashali apata ajali

* Pambano lake la Mei Mosi na Karama Nyilawila lasongezwa mbelele
Bondia Thomasi Mashali akiwonesha waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, majeraha aliyoyapata baada ya kupata ajali hivi karibuni. (Picha zote kwa hisani ya superdboxingcoach.blogspot.com)
Bondia Thomasi Mashali akionesha majeraha aliyoyapata baada ya kupata ajali hiyo.
Jeraha likionekana kwa karibu kwenye mkono wa bondia Mashali.
Bondia Thomasi Mashali akionesha jeraha alilolipata baada ya kupata ajali hivi karibuni.
Bondia Thomas Mashali pichani.
Bondia Thomas Mashali (wa tatu kushoto) akiwa na baadhi ya ndugu na jamaa akiuguza majeraha ya vidonda baada ya kupatas ajarli hivi karibuni.
Bondia Thomas Mashali akionesha majeraha.
Na Mwandishi Wetu BONDIA Thomas Mashali amepata ajarli ya gari mara baada ya kuangukia mtaroni akiwa anaendesha gari aina ya vitz lenye namba za usajili T 777 BMW ajari hiyo iliyotokea maeneo ya Kimara Baruti siku ya April 2o, 2014, wakati akitokea Manzese kwenda nyumani kwake Kimara Mwisho.
 
Akielezea tukio zima la ajali hiyo, Mashali alisema kuwa alikuwa akiendesha mwenyewe gari hilo ambapo alikutana na tuta na kuliruka.
"Nilivyomaliza tu tuta kumbe mbele yangu kulikuwa kumefungwa kutokana na matengenezo ya barabara ya Morogoro, ile nataka kukwepa uzio ambapo upande niliokwepea nikaingia mtaroni moja kwa moja", alisema
Alisema kuwa katika gari hilo, walikuwa wawili, yeye pamoja na mdogo wake, George Maluma, ambaye hakuumia sehemu yoyote katika ajali hiyo.
Akizungumzia mchezo wake, unao mkabili, ambao ulikuwa ufanyike siku ya Mei Mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba kwa ajili ya kumkabili Karama Nyilawila, Mashali alisema kuwa kwa sasa hafanyi mazoezi kwa kuwa anauguza majeraha aliyoyapata katika ajali hiyo, ambapo alisema amechubuka ngozi katika mkono wake wa kulia na ubavuni.

"Namwambia Karama kuwa kafara lake limegonga mwamba hivyo akaye tayari kwa kipigo cha mbwa mwizi kama nilivyo mfanya mwenzie Mada Maugo", alisema

"Kwani na yeye alikuwa anachonga sana lakini mwisho wa siku nikachukuwa ubingwa kupitia kwake yeye mana mpambano huu nilikuwa nausubili kwa hamu kubwa sana", aliongeza Mashali.

Mbali na majeraha hayo alisema kuwa anapenda kuwashukuru baadha ya watu waliomsaidia  katika tukio zima la yeye kupata ajali na kumsaidia kutoa gari lake bondeni ambapo mpaka sasa lipo katika mikono salama, ingawa limeharibika kwakutokana na  kubondeka.

Pia alisema pamoja na hayo anamshukuru promota wake, Ally Mwazoa kwa kuwa na moyo wa huruma na kuamua kusogeza mbele mpambano wao huo mpaka utakapotangazwa tena, pia akawaomba Watanzania wamuombee dua ili aweze kupona haraka majeraha yake ili aweze kuendelea na shughuli zake za kila siki.

No comments:

Post a Comment