Haya ni miongoni mwa matatizo yanayozikabili kampeni kampeni za Jimbo la Chalinze, Kata ya Mandera. Gari likiwa limeacha njia kutokana na utelezi wa barabara.
Mgombea wa Ubunge katika Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete, akicheza ngoma na mmoja wa wazee wa Kata ya Pera, wakati wa kampeni hizo leo.
Mgombea wa Ubunge katika Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete, akifurahi na wakazi wa Kata ya Bwilingu.
Wananchi, wakazi wa Kata ya Lugoba, wakisikiliza hotuba iliyokuwa ikitolewa na Mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete, wakati alipofika katika Kata hiyo leo.
Mkoa wa Vyuo Vikuu, wakiwa bega kwa bega na Mgombea wa Ubunge katika Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete, katika kufanikisha ushindi kwa CCM Chalinze.
Kila mwenye uwezo wa kucheza alicheza siku ya ufunguzi wa kampeni.
Mgombea wa Ubunge katika Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete, akitambulishwa wakati wa mkutano wa kampeni jimboni humo.
RIDHIWANI ajinadi kwa sera safi za utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM. Tangia ameanza Kampeni hajawahi hata siku moja kuzungumzia upinzani, ametumia muda mwingi kuzungumzia maendeleo ya Jimbo la Chalinze.
Viongozi mbalimbali wa CCM na Jumuiya zake waja kumuunga mkono Chalinze.
Tofauti na wagombea wa Vyama vingine Ridhiwani ameweza kufika kila kata ,kijiji kwa kijiji kitongoji kwa kitongoji.
No comments:
Post a Comment