Msemaji Mkuu wa Wizara ya Fedha, Ingiahedi Mduma, akizungumza wakati wa Semina maalum kwa 'Mablogger', iliyofanyika katika Hoteli ya Kilimanjaro Park, Misugusugu Kibaha, juzi Machi 28, 2014. Semina hiyo imeandaliwa na Wizara ya Fedha kwa lengo la utaratibu wa kutimiza utekelezaji wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now).
Na mwandishi wetu, Kibaha
SERIKALI imekusanya jumla ya shilingi bilioni 215.0 katika kipindi cha Julai hadi Disemba, 2013 kutokana na hatua mpya za kodi zilizoibuliwa kwenye maabara za “Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa” yaani Big Results Now (BRN), utaratibu unaotumiwa na Serikali katika kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa baadhi ya majukumu yake kwa lengo la kupata matokeo makubwa kwa muda mfupi.
Haya yamo katika taarifa aliyoitoa msemaji mkuu wa wizara ya Fedha Bi. Ingiahedi Mduma, alipokuwa akitoa taarifa ya utaratibu huo kwa wanablogu, katika kikao maalum na wadau hao, kilichofanyika nje kidogo ya Mkoa wa Pwani, maeneo ya Misugusugu juzi.
Bi. Mduma alisema kuwa Wizara ya Fedha ni miongoni mwa Sekta zinazotekeleza utaratibu huu hususan katika eneo la utafutaji wa mapato (Resource mobilization), sekta nyingine ni Elimu, Kilimo, Maji, Uchukuzi na Nishati.
Utekelezaji wa kila sekta unazingatia viashiria vilivyoibuliwa katika uchambuzi wa kimaabara ulioratibiwa na Serikali kwa kushirikiana na wataalam kutoka nchini Malaysia.
Alisema, "utaratibu huu unaiwezesha Serikali kuongeza ufanisi katika kusimamia utekelezaji wa majukumu yake ikiwemo usimamiaji wa miradi kwa kuweka wazi malengo yaliyokusudiwa pamoja na kuainisha viashiria vya utekelezaji ili kuongeza uwajibikaji kwa kila mshiriki".
Aidha, aliongeza kuwa viashiria hivyo, hutumika kupima hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa maeneo ya kipaumbele na hivyo kuweza kupima mafanikio yaliyopatikana.
Pia, alisema kuwa utaratibu huo, unasaidia kurekebisha mapungufu katika utekelezaji kwa kuchukua hatua mapema na hivyo kuwezesha upatikanaji wa matokeo makubwa kwa haraka.
Bi. Mduma alitanabahisha kuwa wizara yake, imedhamiria kutafuta mapato ya ziada, kiasi cha shilingi trilioni 3.8 hadi kufikia mwaka 2015/16.
Baadhi ya 'Mablogger', wakiwa bize wakati wa semina hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Park, Misugusugu Kibaha.
Baadhi ya 'Mablogger', wakiwa bize wakati wa semina hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Park, Misugusugu Kibaha.
Baadhi ya 'Mablogger', wakiwa bize wakati wa semina hiyo, iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Park, Misugusugu Kibaha. Wa tatu kushoto ni Msemaji Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Ingiahedi Mduma.
No comments:
Post a Comment