TANGAZO


Thursday, December 19, 2013

Vodacom yafungua duka Kibaha

.Ni katika mkakati wa kusogeza huduma zake karibu na wateja

.Kutoa huduma za usajili wa laini, swim swap, M-pesa na mauzo ya simu na modem

Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Vodacom Hassan Saleh akimlaki Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Halima Kihemba wakati akiwasili kwenye hafla ya uzinduzi wa duka jipya la huduma kwa wateja la kampuni hiyo lililopo Maili Moja Mjini Kibaha. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim. Duka hilo linatoa huduma zote za mtandao wa Vodacom ikiwemo usajili wa laini, siwm swap, M-pesa pamoja na mauzo ya simu na modem
Kutoka Kushoto Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Halima Kihemba, Mkuu wa Moa wa Pwani Mwantumu Mahiza , Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Hassan Saleh, Diwani wa Kata ya Maili Moja, na Mkuu wa Usimamizi wa Maduka ya Vodacom Upendo Richard kwa pamoja wakigongesha glass mara baada ya kuzinduliwa kwa duka la Vodacom lililopo Maili Moja Kibaha.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza (katikati), Mkuu wa Wilaya ya
Kibaha Halima Kihemba (kushoto) na Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa
Vodacom Hassan Saleh, wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa
Vodacom na watumishi wa duka jipya la Vodacom Kibaha, mara baada ya
kuzinduliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa huyo.
 
Na Mwandishi wetu
WATEJA wa Vodacom wanaoishi katika Mji wa Kibaha na vitongoji vyake sasa hawalazimiki tena kusafiri hadi Dar es salaam kufuata huduma za mtandao huo wa simu za mkononi unoongoza nchini kufuatia Vodacom kufungua duka jipya lililopo eneo la Maili Moja, Kibaha.
Hilo ni duka la 74 la huduma kwa watja la kampuni hiyo huku maduka mengi zaidi yakiwa karibuni kufunguliwa sehemu mbalimbali hapa nchini kwa lengo la kuwapunguzia mzigo wa gharama wateja kufauta huduma hizo mbali na maeneo wanamoishi.
Akifungua duka hilo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mwantumu Mahiza amesema ni faraja kubwa kuona Vodacom ikitambua umuhimu wa kuweka huduma zake katika mji wa Kibaha kwa kufungua duka kubwa na la kisasa huku akitoa rai kwa wateja kulitumia ili kufikia lengo la kufunguliwa kwake.
“Mji wa Kibaha ni miongoni mwa miji inayokua kwa kasi na yenye shughuli nyingi za kijamii na kiuchumi, hivyo maamuzi yenu ya kufungua duka hapa ni ya msingi na ninawapongeza sana kwani kama ilivyo kwenye maeneo mengine, wakazi wa mji wa Kibaha na vitongoji vyake wangependa kuona kuwa nao wanahudumiwa kwa karibu zaidi.”Alisema Mkuu wa Mkoa
Bi Mahinza amesema kuwa duka hilo sio tu litakuwa msaada mkubwa kwa wenyeji wa Kibaha bali pia wote ambao wanautumia mji wa Kibaha wakiwemo wasafiri na wafanyabiashara.
Amesema kwa ukubwa wa mtandao wa Vodacom ni jambo jema kuhakikisha huduma zake zinakuwa karibu na wananchi kwani kwa kufanya hivyo kunawawezesha kupata suluhu ya changamoto wanazokabiliana nazo ndani ya muda mfupi na hivyo kuwawezesha kuokoa muda na kupunguzia gharama na usumbufu wa kufuata huduma nje ya Mkoa  
“Hili ni duka la kwanza kwenye mkoa wa Pwani na mmesema kuwa mnaendelea na juhudi za kufungua maduka mengi zaidi mkoani humu, nawaomba sana mharakishe kazi hiyo ili wateja wenu katika Mkoa wa Pwani nao waweze kuhudumiwa kwa ukaribu zaidi na pia wanufaike na huduma zenu ikiwemo ya M-pesa ambayo tayari imeshaleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi na kijamii hapa nchini..”Aliongeza
Mkuu huyo wa Mkoa amesema kupitia huduma ya M-pesa sasa maisha yamekuwa rahisi kwani kuna huduma nyingi zimeletwa viganjani mwa watanzania ikiwemo huduma z amsingi za kijamii kama LUKU, kulipia huduma za maji, kulipia ada za shule na vyuo na zaidi kuwawezesha wateja kuweza kutoa na kuweka fedha kwenye akaunti za benki na kusema kuwa hayo ndio maendeleo yanayotakiwa.
Kwa upande wake Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Vodacom Hassan Saleh amesema Vodacom imekuwa katika utekelezaji wa mkakati wake wa kuzisogeza huduma zake karibu zaidi na wateja na kwamba kazi hiyo inaendelea.
“Tunawastani wa kufungua maduka mawli hadi matatu kwa mwezi tangu tulipoanza kazi hii katikati ya mwaka huu tunayafanya yote haya ili kwaondolea wateja wetu vikwazo vya muda na gharama kutufikia.”Alisema Saleh.
“Tunapofungua duka hili hii leo, tayari yapo mengine mengi tu katika hatua za mwisho, ni matumaini yangu kwamba wateja wetu wanayo kila sababu ya kupata huduma bora karibu na kwenye makazi yao.”Alisema Saleh
“Ni vema wateja wetu wakatambua kuwa kasi ya kuwasogezea huduma inazingatia ubora wa huduma mteja anayopata kwenye aaduka yetu yote na kwamba hakuna tofauti katika hilo kati ya duka moja na jengine na hivyo wayatumie kwa kujiamini bila kuwa na hofu ya ubora na aina za huduma zitolewazo”Aliongeza
Amesema uwepo wa maduka mengi kunawapunguza msongamano wa wateja kwenye maduka na kwamba lengo la Vodacom ni kuona kila mteja wake akiwa umbali mfupi na huduma bila kuhitaji usafiri kufikia huduma hizo na akitumia muda mfuopi zaidi kuhudumiwa..
“Lengo letu ni kumpa urahisi mteja wetu na uwezo wakufikia huduma zetu kwa ukaribu. Wateja wa Vodacom ndio mhimili wetu mkubwa kaika biashara hivyo na sisi hatutabaki nyuma kuwapatia urahisi wa upatikanaji wa huduma zetu. Tunatambua mkoa wa Pwani una wafanyabiashara wengi na wakazi wengi wote wakihitaji huduma bora za mawasilisno ya simu kwa shughuli zao za kiuchumi na kijamii,”Aliongeza

No comments:

Post a Comment