TANGAZO


Thursday, December 19, 2013

TUME YA KATIBA KUKABIDHI RASIMU YA KATIBA KWA MHE. RAIS DESEMBA 30 2013

 
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, akiwa na Katibu wake, Assa Rashid.
Hafla ya kukabidhi Rasimu ya Katiba kwa Mhe. Rais
Tume ya Mabadiliko ya Katiba inapenda kuwafahamisha wananchi na wadau wengine wote kuwa Hafla ya kukabidhi Rasimu ya Katiba kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi itafanyika siku ya Jumatatu, Desemba 30, 2013 katika Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam.
Hafla hiyo pia inatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wa Serikali, vyama vya siasa, taasisi za kidini, asasi za kiraia na wananchi wa kawaida. 
Taarifa zaidi kuhusu hafla hii zitatolewa baadaye. 

No comments:

Post a Comment