TANGAZO


Tuesday, November 26, 2013

Wasomi wa CBE, Dar es Salaam wapigwa msasa


Naibu Mkuu wa Chuo Cha Elimu ya Biashara (CBE), Dk. Abby Nangawe akiongea muda mfupi kabla ya kuanza kwa mhadhara wa wazi uliondaliwa na Jumuiya ya Wana-masoko ya wanafunzi wa chuo hicho. Katikati ni Mkuu wa Idara ya Masoko wa Vodacom Kelvin Twissa, ambaye ndiye aliyekuwa mzungumzaji Mkuu Mwaalikwa kwenye mhadhara huo na kulia kwake ni Mkuu wa Idara ya Masoko wa CBE, Godian Bwemelo. Mhadhara huo umefanyika jana, chuoni hapo, jijini Dra es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Masoko wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa akizungumza na Jumuiya ya wana-masoko ya wanafunzi wa chuo cha Elimu ya Biashara  - CBE (COBEMA) chuoni hapo jana. Twissa alikuwa mgeni mwalikwa kwenye mdahalo wa wazi chuoni hapo, kwa ajili ya kubadilishana uzoefu wake katika sekta ya masoko na wanafunzi wa CBE. Vodacom imekuwa ikitumia wafanyakazi wake waliobobea katika fani  mbalimbali kushiriki katika midahalo ya aina hiyo, vyuoni kuwapa uzoefu wa kitaaluma wanafunzi.
Mkuu wa Idara ya Masoko wa Vodacom Kelvin Twissa, akionesha kwa vitendo mbinu za kimasoko, wakati alipoalikwa kuzungumza na Jumuiya ya wana-masoko ya wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara - CBE (COBEMA), chuoni hapo jana. Twissa ni mmoja kati ya vijana waliobobea katika nyanja ya masoko na matangazo nchini na alialikwa chuoni hapo kubadilishana uzoefu wake katika sekta hizo na wanafunzi wa CBE. Vodacom imekuwa ikitumia wafanyakazi wake, waliobebea katika fani mbalimbali kushiriki katika midahalo ya aina hiyo, vyuoni kuwapa uzoefu wa kitaaluma wanafunzi. (Picha zote na mpigapicha wetu)

*Watakiwa kuchangamkia fursa za ajira

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Mamia ya wanafunzi wa chuo cha Elimu ya Biashara CBE wamepata mafunzo ya ujasiriamali na kuchangamkia fursa za masoko katika kujiendeleza kiuchumi.

Akizungumza katika mdahalo ulioandaliwa na jumuia ya Wana Masoko ya wanafunzi wa chuo cha elimu ya Biashara CBE Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa amesema wasomi wengi wa vyuo wanayonafasi ya
kujiajiri kuliko kutegemea ajira serikalini endapo watajijengea uwezo tangu wakiwa vyuoni kupitia vyama vyao.

" Hatupaswi kutegemea ajira kutoka serikalini au sekta binafsi, Mkiwa chuo mnatakiwa kuanzisha vyama kama hivi na kuhakikisha mnatafuta fursa za kuungana na taasisis mbalimbali ambazo zinaweza kuwapatia mikopo na kuanzisha miradi ambayo
itawajengea uwezo na kujiendeleza mnapo maliza chu" alisema Twissa na kuongeza.

"Kama mwanafunzi ukijenga hali ya kujiamini tangu mwanzo na kuhakikisha hauachi kila fursa inayojitokeza ni rahisi kufanikiwa na kujiendeleza zaidi, wito wangu kwa wanafunzi wa chuo hichi na wengineo nchini ni kuhakikisha wanajenga msingi bora wa
kujitengenezea ajira wakiwa badi vyuoni, hili linawezekana kwa kuwashirikisha wadau wengine, kama sisi Vodacom na wadau wengine."

Kwa upande wake Naibu Mkuu wa Chuo Cha Elimu ya Biashara (CBE) Dr. Abby Nangawe, amesema wataendelea kuunga mkono jitihada za wanafunzi wa chuo hicho katika kushirikiana na wadau mbalimbali kutengeneza fursa za ajira na kujijengea uwezo, huku
akitoa pongezi kwa umoja wa chama cha wanamasoko wa chuo hicho kwa kufanikisha mdahalo huo.

Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho wamesema wamefurahishwa na moyo wa kujitolea walionao kampuni ya Vodacom kwa kushirikiana nao katika kuwakomboa wanafunzi nchini huku wakipongeza huduma zinazo anzishwa na kampuni
hiyo katika kuwawezesha wanafunzi kuwasiliana kwa bei nafuu.

"Tunawashukuru Vodacom kwa kuanzisha huduma yao ya Happy Hour ambayo inatuwezesha wanafunzi tusio na kipato kuweza kuwasiliana kwa bei nafuu na wanafunzi wenzetu, alisema Gloria Tesha moja ya wanafunzi wa chuo hicho na kuongeza.

"Tutaendelea kushirikiana na kampuni hii kama wao wanavyoshirikiana nasi na tutaendelea kuwaunga mkono kutokana na huduma zao kwetu sisi wanafunzi, ombi letu kwa kampuni hii ni kuiwezesha huduma hii ya Happy Hour kuwa ya Masaa 24 kwa sababu muda wa mchana wengi tunakuwa darasani." Alisema Tesha.

No comments:

Post a Comment