TANGAZO


Tuesday, November 26, 2013

Unyanyapaa kwa vijana walio na HIV

 

Kampeini dhidi ya maambukizi ya HIV kwa vijana
Shirika la afya la Umoja wa Mataifa limekosoa kile linachosema ni kutowajali na kutowasaidia vijana wanaoishi na virusi vya HIV , vinavyosababisha ugonjwa wa ukimwi.
 
Likiwataja vijana hao kama kikundi cha watu waliotengwa, WHO limesema kuwa vijana wengi hawapati msaada wanaohitaji ili kujiweka katika hali nzuri ya kiafya na kuzuia maambukizi.

Inaarifiwa katika zaidi ya vijana milioni mbili walio kati ya umri wa miaka 10 na 19 wanaishi na virusi vya HIV. Idadi hii inasemekana imeongezeka kwa thuluthi moja katika miaka kumi iliyopita.

Craig McClure wa shirika la kushughulikia maslahi ya watoto la UNICEF, amesema kuwa sheria kali, kutengwa , ubaguzi na unyanyapaa ni vikwazo vikuu katika kuzuia matibabu na kuzuia kuambukizwa upya.

Aliongeza kuwa ikiwa vikwao hivyo havitaondolewa huenda, ndoto ya kuangamiza virusi vya HIV ikatumbukia nyongo.

No comments:

Post a Comment