Waandamanaji katika mji mkuu wa Thailand, Bangkok wameendelea
kulenga wizara za serikali, wakidhibiti baadhi ya majengo na mengine
kuyazingira, wakipinga utawala wa waziri mkuu, Yingluck Shinawatra.
Waandamanaji wanasema wanalenga kukwamisha shughuli za serikali kwa lengo la kumlazimisha waziri mkuu kujiuzulu.
Wanasema Bi Yingluck ni kibaraka wa kaka yake, Thaksin Shinawatra ambaye alikuwa waziri mkuu wa zamani wa Thailand aliondolewa madarakani kwa njia ya maandamano.
No comments:
Post a Comment