TANGAZO


Tuesday, November 26, 2013

Hali yatulia Jimbo la Turkana, Kenya

 

Jamii za Pokot na Turkana zimekua zikizozania maliasili kwa manufaa ya mifugo wao.
 
Polisi nchini Kenya wamesema kua hali ya utulivu imerejea katika kijiji kilichokuwa kimezingirwa na wavamizi kutoka jamii hasimu katika jimbo la Turkana Kaskazini Magharibi mwa Kenya.
 
Washambulizi walivamia kijiji cha Klooigon kilichokuwa na karibui wakaazi 900 ambao walizuia kuondoka.
 
Wavamizi kutoka jamii ya Pokot walizingira kijiji cha Lorokon, nyumbani kwa jamii ya waturkana.

Waliteka vituo vitatu vya polisi na kuweka vizuizi barabarani ili kuzuia vikosi vya usalama kuingia katika kijiji hicho huku wakikabiliana vikali na polisi waliofika kudhibiti hali, Jumamosi na Jumapili.
Msemaji wa Polisi alisema kuwa hali ilitulizwa baada ya viongozi wa jamii hizo mbili ambazo huzozania mali asili mara kwa mara kuingilia kati na kuwashawishi wavamizi kuondoka kutoka eneo hilo.
Duru zinasema kuwa hakuna mtu alijeruhiwa na kuwa polisi wangali wanaondoa vizuizi vilivyo kua vimewekwa barabarani ili kuwazuia kuingia katika kijiji hicho.

Maafisa wa utawala waliweka sheria ya kutotembea usiku mnao siku ya Jumamosi baada ya wavamizi kuingia Lorogon.

Shirika la msalaba mwekundu linakadiria kuwa karibia watu 600 hadi 900 walikuwa katika kijiji hicho, kilichokuwa kimezingirwa na wavamizi 150.

Kwa mujibu wa shirika hilo, hali ilianza kutokota mwezi Novemba tarehe 18 baada ya watu wawili wa jamii ya Pokot kuuawa,mauaji ambayo waturkana walidaiwa kuyatekeleza.

Katika hali ya kulipiza kisasi, watu wa jamii ya Pokot nao wakaamua kuwashambulia waturkana.

Jamii hizo mbili zimekuwa zikizozana hasa kuhusu malisho ya mifugo wao.

No comments:

Post a Comment