Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Meja Generali Mstaafu Ligate
Sande akitoa hotuba katikamahafali ya 9 ya Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI). (Picha zote na Hussein Makame, Ofisa Habari, Idara ya
Habari-MAELEZO)
Ndudu na jamaa wa wahitimu wakifuatilia hotuba ya Mwenyeki.Baadhi ya wahitimu katika ngazi mbalimbali wakimsikiliza Mwenyekiti wa bodi ya Chuo.
Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 9 ya DMI Katibu Mkuu wa
Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaabani Mwinjaka akihutubia katika mahafali hayo.
Baadhi ya wahitimu katika ngazi mbalimbali wakimsikiliza Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 9 ya DMI Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaabani Mwinjaka wakati alipokuwa akihutubia katika mahafali hayo.Baadhi ya wahitimu katika ngazi mbalimbali wakimsikiliza Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 9 ya DMI Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaabani Mwinjaka wakati alipokuwa akihutubia katika mahafali hayo.
Baadhi ya wahitimu katika ngazi mbalimbali wakimsikiliza Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 9 ya DMI Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaabani Mwinjaka wakati alipokuwa akihutubia katika mahafali hayo.
Baadhi ya wahitimu katika ngazi mbalimbali wakimsikiliza Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 9 ya DMI Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaabani Mwinjaka wakati alipokuwa akihutubia katika mahafali hayo.
Mgeni Rasmi Dk. Mwinjaka akimtunuku Cheti Mhitimu wa Stashahada ya Juu ya Usafirishaji wa Majini (ADMT), Dilshad Murtaza kwa kupata Daraja la Kwanza la GPA 4.5 kwenye Kozi hiyo.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Mipango, Fedha na Utumishi, Dk.
Tumaini Gurumo akimkabidhi Mgeni Rasmi zawadi aliyoandaliwa na chuo hicho.
Hussein Makame, MAELEZO
CHUO
cha Bahari Dar es Salaam (DMI), kimejipanga kutoa elimu ya rasilimali
za baharini ikiwemo mafuta na gesi katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na
dunia kwa ujumla.
Hayo
yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DMI, Meja Generali
Mstaafu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ); Ligate Sande katika
mahafali ya 9 ya chuo hicho, yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti
huyo, alisema wamefikia hatua hiyo ili kuifanya Tanzania ambayo ni nchi iliyoko
ukanda wa bahari wenye wingi wa rasilimali ya mafuta na gesi kunufaia na
rasilimali hizo.
Alisema
moja ya kigezo cha kuboresha na kusimamia rasilimali baharini na maeneo
yanayozunguka bahari ni kuwa na rasilimali watu ya kutosha na yenye ujuzi na
weledi katika mambo ya bahari.
Meja
General Mstaafu Sande alisema pamoja na kuwa na rasilimali watu ya kutosha kunahitajika
mikakati ya makusudi ili kuifanya Sekta
ya bahari iwe endelevu na yenye tija kwa Taifa.
“DMI
imejipanga katika kutoa elimu ya aina hii katika ukanda huu wa Afrika Mashariki
na kati na dunia kwa ujumla” alisema mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa chuo
hicho ambacho ni Kituo cha Ubora (Centre of Excellency) wa Elimu ya Bahari
inayotambuliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Akizungumzia
changamoto zinazikikabili chuo hicho, mwenyekiti huyo alisema pamoja na
changamoto nyingine, DMI kina uhaba wa miundombinu ya madarasa na ofisi za
walimu katika kukidhi mahitaji ya ongezeko la wanafunzi wanaojiunga na chuo
hicho kutoka nchi mbalimbali barani Afrika.
Akizungumzia
changamoto hizo, Mgeni Rasmi kwenye Mahafali hayo Katibu Mkuu wa Wizara ya
Uchukuzi Dk. Shaaban Mwinjaka alisema
anatambua umuhimu
wa DMI na changamoto zinazokikabili.
“Hata hivyo ninatambua kuwa DMI inao uwezo wa kutoa
mchango wa wataalamu katika fursa hizo hususan waendesha meli, Wahandisi wa
meli, Uchimbaji gesi na Mafuta, Usafirishaji shehena, Ukarabati wa meli, Ajira
ndani na nje ya nchi” alisema Dk Mwinjaka.
Katika mahafali hiyo yenye kauli mbiu isemayo Sekta ya
Bahari “Matokeo Makubwa Sasa” Zingatia Elimu Bora na Usawa Kijinsia”, yalishuhudia
wahitimu 403 wakitunukiwa vyeti kwa ngazi ya Stashahada ya Juu, Stashahada na
Cheti.
Mbali na tunu hizo,
wahitimu 10 walitunukiwa vyeti kutokana na kufanya vizuri kwenye masomo katika
mwaka wa masomo wa 2011/2012 na 2012/2013 akiwemo Dilshad Murtaza aliyepata
Daraja la Kwanza la ufaulu wa GPA ya 4.5 katika Shahada ya Juu ya Usafirishaji
wa Majini (ADMT).
No comments:
Post a Comment