Mahakama maalumu ya Bangladesh ya kusikiliza uhalifu wa vitani
yametoa hukumu ya kifo kwa Wabangladeshi wawili walioko uhamishoni, kwa
kushiriki kwenye mauaji ya wasomi na waandishi wa habari 18.
Upande wa mashtaka uliiambia mahakama mjini Dhaka kwamba Chowdhury Mueen-Uddin - ambaye sasa anaishi Uingereza - na Ashrafuzzaman Khan - sasa raia wa Marekani - walikuwa katika kundi la wanamgambo ambalo likiunga mkono jeshi la Pakistan.
Wanaume hao wawili walifanyiwa kesi bila ya kuwepo na wamekanusha mashtaka hayo.
Serikali iliwapatia mawakili kuwatetea ingawa hakuna shahidi aliyeitwa kwa upande wao.
No comments:
Post a Comment