TANGAZO


Thursday, October 31, 2013

Warsha ya pamoja ya Sekta ya Nishati yafanyika jijini Dar es Salaam

Baadhi ya washiriki wa warsha ya pamoja kwa wadau wa sekta ya Nishati wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakimu Maswi  (hayupo pichani) wakati akifungua mkutano wa saba uliofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency  iliyopo jijini Dar es Salaam. Serikali imekamilisha utafiti katika  vituo 52 vya kutoa umeme wa joto ardhi (geothermal) na ifikapo mwakani uchimbaji wa umeme huo utaanza katika vituo vitatu vilivyopo katika mkoa wa Mbeya, wilaya ya Rufiji na katika ziwa Natroni lililo  mkoani Manyara.
Baadhi ya washiriki wa warsha ya pamoja kwa wadau wa sekta ya nishati wakimsikiliza Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini Eliakimu Maswi  (hayupo pichani) wakati akifungua mkutano wa saba uliofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency  iliyopo jijini Dar es Salaam. Serikali imekamilisha utafiti katika  vituo 52 vya kutoa umeme wa joto ardhi (geothermal) na ifikapo mwakani uchimbaji wa umeme huo utaanza katika vituo vitatu vilivyopo katika mkoa wa Mbeya, wilaya ya Rufiji na katika ziwa Natroni lililo  mkoani Manyara.
Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini Eliakimu Maswi  (kulia) akimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Eng. Ngosi Mwihava (katikati) wakati wa warsha ya pamoja ya siku moja kwa wadau wa sekta ya nishati iliyofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency  iliyopo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kamishina wa masuala ya Nishati na Mafuta Eng. Hosea Mbise.
Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini Eliakimu Maswi  (kulia) akifuatilia mada iliyokuwa inawasilishwa na Dk. Lennart Larsson wakati wa warsha ya pamoja ya siku moja kwa wadau wa sekta ya nishati iliyofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency  iliyopo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kamishina wa masuala ya Nishati na Mafuta Eng. Hosea Mbise.
Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini Eliakimu Maswi  (kushoto) akiongea na Dk. Lennart Larsson (kulia) mara baada ya ufunguzi wa farsha ya pamoja ya siku moja kwa wadau wa sekta ya nishati iliyofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency  iliyopo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini Eliakimu Maswi  akifungua warsha ya pamoja kwa wadau wa sekta ya nishati leo katika Hoteli ya Hyatt Regency  iliyopo jijini Dar es Salaam. Katika mkutano huo wa saba uliofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency  mambo mbalimbali yalijadiliwa ikiwa ni pamoja na masuala ya mafuta, umeme na gesi.
Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini Eliakimu Maswi (kulia) akiongea jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Eng. Ngosi Mwihava wakati wa  warsha ya pamoja kwa wadau wa sekta ya nishati iliyofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Serikali imekamilisha utafiti katika  vituo 52 vya kutoa umeme wa joto ardhi (geothermal) na ifikapo mwakani uchimbaji wa umeme huo utaanza katika vituo vitatu vilivyopo katika mkoa wa Mbeya, wilaya ya Rufiji na katika ziwa Natroni lililo  mkoani Manyara. (Picha zote na Anna Nkinda - Maelezo)

No comments:

Post a Comment