TANGAZO


Monday, October 28, 2013

Rais Kikwete na mkewe watoa pole kwa mjane na familia ya Balozi Isaac Sepetu

                 
        w1
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa pole mjane wa Balozi Isaac Sepetu, Mama Miriam Sepetu, alipokwenda na mkewe, Mama Salma, nyumbani kwa marehemu, Sinza Mori, Dar es Salaam, kutoa pole kwa mjane huyo na familia ya marehemu Sepetu aliyefariki jana jijini Dar es Salaam. w2
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akitoa pole kwa wanafamilia wa Balozi Isaac Sepetu, alipokwenda na mkewe, Mama Salma nyumbani kwa marehemu Sinza Mori, Dar es salaam, kutoa pole kufuatia msiba wa marehemu Sepetu aliyefariki jana jijini Dar es Salaam. w3
Mke wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma, akimfariji mjane wa Balozi Isaac Sepetu, alipokwenda  nyumbani kwa marehemu, Sinza Mori, Dar es Salaam, kutoa pole kufuatia msiba wa marehemu Sepetu, aliyefariki jana jijini Dar es Salaam. w4
Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa Balozi Isaac Sepetu alipokwenda  nyumbani kwa marehemu, Sinza Mori, Dar es Salaam, kutoa pole. Marehemu Sepetu alifariki jana, jijini Dar es Salaam. w5
Mama Salma Kikwete, akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa Balozi Isaac Sepetu  nyumbani kwa marehemu Sinza Mori, Dar es Salaam. Marehemu Sepetu alifariki jana jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment