TANGAZO


Tuesday, September 17, 2013

Rais Dk. Jakaya Kikwete afungua Ofisi ya Ubalozi wa Heshima jijini San Francisco, nchini Marekani


Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi Ofisi ya Ubalozi wa Heshima (Honorary Consulate) wa Tanzania jijini San Francisco, nchini Marekani leo jioni. Kulia ni Balozi wa heshima wa Tanzania jijini San Francisco, Ahmed Issa, kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Liberata Mulamula na wapili kushoto ni mke wa Balozi Issa, Mama Sherry Julin Issa.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Heshima wa Tanzania jijini San Francisco, Ahmed Issa (wapili kushoto), muda mfupi baada ya kufungua Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania jijini San Francisco nchini Marekani leo jioni. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Liberata Mulamula na kulia ni mke wa balozi Issa, Mama Sherry Julin Issa.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya Watanzania waishio jijini San Francisco, Marekani muda mfupi baadaya kufungua Ubalozi wa Heshima wa Tanzania na kuzungumza nao leo jioni.

Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na baadhi ya Watanzania waishio jijini San Francisco Marekani leo jioni. Rais Kikwete yupo nchini Marekani kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine atahutubia kikao cha 68 cha Umoja wa Mataifa, jijini New York Marekani. (Picha zote na Freddy Maro)                             

No comments:

Post a Comment