Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa, akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa duka la huduma kwa wateja la Vodacom lililoko Msimbazi kariakoo jijini Dar es Salaam. Pamoja nae katika picha ni Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Hassan Saleh kulia na Mkurugenzi wa Planetell David Hayes. Hilo ni duka la 70 la kampuni hiyo nchini.
Ofisa
Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa
Vodacom Tanzania, Hassan Saleh, akimfafanulia jambo Meya wa Manispaa ya Ilala
Jerry Silaa kuhusu mfumo wa uhifadhi wa taarifa za M-pesa zinazowahusu wateja
wakati Meya akiangalia huduma mbalimbali zinazotolewa kwenye duka jipya la
Vodacom Msimbazi mara baada ya kulizindua.Wengine pichani ni Meneja wa duka
hilo Josephine Swai na Mkuu wa kitengo cha Mauzo wa Vodacom.
Ofisa
Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa
Vodacom Tanzania, Hassan Saleh, akifafanua jambo kwa Mstahiki Meya wa manispaa
ya Ilala Jerry Silaa baada ya uzinduzi wa duka jipya la huduma kwa wateja la
Vodacom lililoko Msimbazi karikoo jijini Dar es Salaaa. Pamoja nao kutoka kushoto ni Meneja wa
duka hilo Josephine Swai na Mkuu wa kitengo cha Mauzo wa kampuni hiyo Upendo Richard. Kampuni hiyo imefikisha maduka 70 ya huduma kwa wateja nchini.
Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa (kulia), akisalimiana na Mkurugenzi wa Pantell David Hayes wakati akiwasili kwa ajili ya ufunguzi wa Duka jipya la Vodacom lililoko Msimbazi kariakoo jijini Dar es Salaam, Wanaoshuhudia wa kwanza kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Mauzo wa kampuni hiyo Upendo Richard, Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Hassan Saleh na Meneja uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim.
Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mfanyakazi wa wa duka jipya la Vodacom Msimbazi namna huduma zinavyotolewa kwa wateja wa kampuni hiyo. Wa kwanza kulia ni Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Hassan Saleh. Meya Silaa alilizundua rasmi duka hilo.
Ofisa
Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa
Vodacom Tanzania, Hassan Saleh, (wa kwanza kushoto) akimueleza Meya wa manispaa ya Ilala Jerry Silaa
namna duka hilo linavyotoa huduma kwa wateja mara baada ya uzinduzi wa duka jipya la huduma kwa wateja la
Vodacom lililoko Msimbazi karikoo jijini Dar es Salaaa. Pamoja nao katika ni Meneja wa uhusiano
wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim, na Mkurugenzi wa Pantell David Hayes.
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Ukuaji na uimarikaji wa matumizi ya huduma za fedha mtandao nchini umekuwa wenye umuhimu mkubwa kwa uchumi w anchi kwa hivio sasa ambapo kiasi kikubwa cha mzunguzko wa fedha za shughuli za kiuchumi na kijamii zimekuwa zikitegemea huduma hizo na kuchangia ukuaji wa uchumi.
Hayo yamesemwa na Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa wakati wa uzinduzi wa duka jipya la Vodacom Msimbazi jijini Dar es salaam ambapo alitumia fursa hityo kusifu juhudi za Vodacom katika kuimarisha huduma zake ikiwemo ya M-pesa na kuziletea karibu na wateja huduma zake zote.
Meya Silaa amesema kwa kiasi mzunguko wa uchumi kwa sasa unategemea huduma za pesa mtandao unaotumia teknolojia ya simu za mkononi ambapo huduma ya M-pesa imekuwa ikiongoza soko huku akielezea jinsi ambavyo uwepo wa duka hilo kwenye eneo ambalo ni kitovu cha biashara kwa nchi za maziwa makuu litakavyochangia uchumi wa nchi na ustawi wa biashara.
"Hivi sasa kuna matumizi makubwa ya huduma za fedha mtandao ambapo kila mmoja amekuwa akitumia huduma hizo kwa ajili ya shughuli za kibiahara na kiuchumi huku tukiona M-pesa inavyoongoza soko kwa hiyo tunaposhuhudia zuinduzi wa maduka kama haya ni dhahiri kuwa tunaongeza matumizi ya huduma hizo."Alisema Meya Silaa.
"Msimbazi ni kitovu cha kikuu cha baishara sio tu kwa Tanzania bali kwa nchi za maziwa makuu hivyo ni jambo lisoepukika kuwa na maduka ya huduma kwa wateja ambayo yanafanya upatikanaji wa huduma kuwarahisi na kwa kwa unafuu"
Hata hivyo Meya Silaa amesema ukuaji wa baishara kwney sekta binafsi unatoa changamoto kwa seriklai na halmashauri kuona ni jinsi gani mipango wanayoiweka nayo pia iankwenda na kasi inayofanana.
"Miji yetu inakuwa kwa kasi na wenzetu kwenye sekta binafsi wanavyoweka mikakati ya kufikisha huduma zake karibu zaidi na wannachi tumesikia Vodacom wamefungua duka Gongolamboto hii maana yake kwamba hata mipango yetu sisi nayo inahitaji kuboreshwa penye Zahanati tuweke kituo cha afya huku tukipunguza ukiritimba."
"Maduka haya yana mchango mkubwa kwa kuwa mbali na kusogeza huduma karibu na wananchi pia yanatengeneza ajira na kukuza biashara ambayo mwisho wa yote ni ulipaji wa kodi ambazo zinakuja kuwa msaada kwa wananchi wote kwa ujumla." Alisema Silaa na kuongeza "Hata hivyo usishnagae kwamba kibali tu cha ukarabati wa jengo hili umechukua mwezi mzima haya ni ammbo ambayo hayakubaliki katika zama za sasa za baishara lazima tupunguze ukiritimba na kuweka mifumo rahisi kwa biashara kwa kuwa zinachangia kwenye kodi."
Kwa upande wake Ofisa Masoko Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa kampuni ya Vodacom Hassan Saleh amesema mapema mwaka huu Vodacom ilijiwekea lengo la kufungua maduka 100 ya huduma kwa wateja ikilenga kuziwezesha huduma zake kuzileta karibu zaidi na wateja kuwawezesha kupata huduma hizo kwa urahisi na kwa gharama nafuu.
Saleh amasema ongezeko la wateja wa Vodacom na ukuaji wa miji nao unachangia kutoa msukumo kwa lengo hilo na kwmaba duka la Msimbazi ni la 70 kwa Vodacom nchi nzima na la 18 kwa mkoa wa Dar es salaam na kwamba kazi ya kufungua maduka hayo inaendelea nchi nzima.
"Mwaka huu tulijiweka lengo mahsusi la kupeleka huduma zetu karibu zaidi na wateja wetu ikiwemo kufungua maduka haya katikakati ya miji na nje ya miji ili kuwapunguzia usumbufu wateja wetu ambao wamekuwa wakilazimika wakati mwengine kufuata huduma hizi kwenye maduka yetu ya mbali."Alisema.
"Tunajisikia furaha kubwa kuona tunakwenda vizuri na utekelezaji wa lengo letu, ahadi yetu ni kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja wetu na kwamba kazi hii ya ufunguzi wa maduka inaendelea Dar es salaam na nje ya Dar es salaam."
Saleh amewaomba wannachi kutumia fursa ya uwepo wa maduka hayo mapya karibu na makazi ama shughuli za biashara ili kupata huduma zote za Vodacom na kwamba hakuna ulazima wa wao kufuata huduma hizo kwenye maduka waliyoyazoea ya Mliamni City na Samora.
"Kabla ya maduka haya mapya wengi wa wateja wetu walikuwa wakifuata huduma kwenye maduka machache yaliyokuwepo hii iliwasababishia gharama na usumbufu wa kupanga foleni, hali hiyo kwa sasa haina tena ulazima na tutaendelea kuimaliza kadri tunavyofungua maduka haya mapya." Alisema Saleh.
Katika maduka hayo, huduma zote za Vodacom zinapatikana ikiwemo ya usajili, utatuzi wa matatizo ya kiufundi ikiwemo ya data, huduma za M-pesa na nyinginezo.
No comments:
Post a Comment