TANGAZO


Tuesday, September 17, 2013

Kampuni ya Platinum Credit yasaidia vifaa vya michezo kwa ajili ya mashindano na Shimiwi

Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya Platinum Credit Ltd, Bw. Elias Samwel akimkabidhi moja ya jezi, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Magereza Mkwanda Hassid leo, jijini Dar es Salaam ikiwa ni mchango wa kampuni katika kusaidia mashindano ya Shimiwi yanayotarajia kuanza hivi karibuni mjini Dodoma. Kushoto ni Mratibu Masoko, Richard Rwegasira na Meneja Masoko, Ferdinand Kambanyuma.


Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya Platinum Credit Ltd, Bw. Elias Samwel akimkabidhi moja ya jezi, Katibu wa Klabu ya Michezo ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bw. Saidi Marusu leo, jijini Dar es Salaam, ikiwa ni mchango wa kampuni hiyo katika kusaidia  mashindano hayo, ya Shimiwi yanayotarajia kuanza hivi karibuni, mjini Dodoma. Kushoto ni  Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Ferdinand Kambanyuma.
Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Mkwanda Hassid  akitoa neno la shukrani kwa kampuni ya Platinum Credit Ltd, kwa kuwapatia msaada wa vifaa vya michezo, ambavyo ni jezi, T- shirt na kofia, katika hafla iliyofanyika leo, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni  hiyo, Bw. Elias Samwel.
Mwakilishi wa TAMISEMI ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Shimiwi, Bw. Ramadhani Sululu akitoa neno la shukrani kwa Kampuni ya Platinum Credit Ltd, baada ya kukabidhiwa vifaa vya michezo kwa ajili ya mashindano ya Shimiwi yanayotarajiwa kuanza hivi karibuni mjini Dodoma. Wa kwanza  kushoto ni Meneja Masoko, Ferdinand Kambanyuma na katikati ni Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni  hiyo, Bw. Elias Samwel.

Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni  ya Platinum Credit Ltd,  Bw. Elias Samwel (wa pili kutoka kushoto), akiwa na wawakilishi kutoka Magereza, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo  na Meneja Masoko wa kampuni hiyo, wakionyesha vifaa vya michezo walivyovikabidhi leo, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya Shimiwi yanayotarajiwa kuanza hivi karibuni mjini Dodoma. (Picha zote na Lorietha Laurence).

No comments:

Post a Comment