TANGAZO


Tuesday, September 17, 2013

Shirika la IDYDC lamwaga mipira yenye thamani ya Tsh. milioni 250 mashuleni Iringa


Naibu  Meya  wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Gervas Ndaki (kushoto), akimkabidhi mpira Mwalimu Mkuu  wa  Shule ya Msingi Kihesa, Zabihu Hassan, mjini humo jana. Jumla ya mipira  5000, yenye  thamani ya sh. milioni 250   imetolewa na Shirika la IDYDC kwa  vijana waliopo mashuleni na nje ya  shule  ili kuwaepusha na matumizi ya dawa  za kulevya. (Picha na Francis Godwin)

Na Francis Godwin, Iringa
SHIRIKA  lisilo la kiserikali linalojihusisha na masuala mbali  mbali yakiwemo  ya  elimu  kwa  vijana (IDYDC) limemwaga  mipira 5000 yenye thamani  ya Tsh milioni 250 kwa  shule  za msingi na vijana  waliopo nje ya  shule kwa ajili ya kuendeleza mapambano  dhidi ya madawa  ya  kulevya.
Akimkaribisha  mgeni  rasmi Naibu Meya  wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa  Gervas Ndaki kukabidhi mipira  hiyo, mratibu  wa mradi  wa vijana Naomi Nyalusi .
  Alisema  kuwa mipira  hiyo  itatolewa  kwa  shule  zote za Manispaa ya  Iringa na kila  shule  itapewa mipira  nane na  kuwa  kila mpira  mmoja unauzwa dola  30 na  kuwa mipira  hiyo ni imara na ya kisasa  zaidi haihitaji kujazwa  upepo kwa kutumia pampu  za kawaida bali inajijaza yenyewe kwa upepo.

Hata  hivyo alisema  kuwa vijana  wanaolengwa na mradi  huo wa vijana ni  wale  wenye  miaka kati ya 14 -18  ambao  wapo mashuleni na  waliopo nje ya  shule.

Nyalusi  alisema  kuwa utafiti  uliofanywa na IDYDC ambao  pia ni wamiliki wa  kituo cha Radio  Nuru Fm unaonyesha  kuwa asilimia  zaidi ya  30 ya  vijana  waliopo mashuleni wanatumia madawa  ya  kulevya  ikiwemo  pombe .

Hivyo  alisema njia  pekee  ya  kuwaepusha  vijana hao na matumizi ya  pombe na dawa  za kulevya ni  kuwawezesha  vifaa vya michezo  ili pindi  wanapotoka  shule  kujikita katika  michezo  zaidi.

Katika  kuhakikisha  vijana  wanawezesha  zaidi katika michezo shirika  hilo kwa ufadhili wa FIFA limeanza  kujenga kituo  cha Michezo kwa vijana.

Kwa  upande  wake mgeni rasmi katika hafla  hiyo Naibu meya  wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa  Gervas Ndaki  mbali ya  kupongeza  jitihada  kubwa  zinazofanywa na IDYDC na kituo  cha Radio  Nuru Fm mkoani Iringa bado alisema  kuwa ni kwa mara ya kwanza Manispaa ya Iringa inapokea  msaada wa mipira  mingi kiasi  hicho .

"Sijapata  kuona  msaada mkubwa kama  huu wa mipira  ukitolewa katika Manispaa ya Iringa ....huu ni msaada wa kwanza mkubwa  kutolewa "

Hata  hivyo  aliwataka  walimu  wakuu wa shule zote za msingi mjini Iringa  kuanza kuandaa viwanja  vya michezo kama  ilivyo  shule ya msingi Nyumbatatu ambapo tayari  wana kiwanja  cha  kisasa.

Akishukuru kwa mipira  hiyo mkuuwa  shule ya msingi Tumain Abel Mkangwa alisema  kuwa jitihada  zilizoonyeshwa na IDYDC ni za kupongezwa na kuwa  wao kama  walimu  wamepunguziwa mzigo wa kununua  mipira kwa ajili ya  kufundishia michezo

No comments:

Post a Comment