Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Habari, Maelezo, Zamaradi Kawawa, akizungumza kabla ya kumkaribisha, Msemaji Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kitengo cha Serikalini, Julian Tendwa, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akielezea kuhusu Mpango wa Taifa wa Kujiandaa Kukabiliana na Majanga na Mkakati wa Mawasiliano wakati wa maafa. Kushoto ni Ofisa Habari wa Ofisi hiyo, Francisca Swai. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Habari, Maelezo, Zamaradi Kawawa, akizungumza wakati alipokuwa akimkaribisha, Kaimu Msemaji Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kitengo cha Serikalini, Julian Tendwa.
Kaimu Msemaji Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kitengo cha Serikalini, Julian Tendwa, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akielezea kuhusu Mpango wa Taifa wa Kujiandaa Kukabiliana na Majanga na Mkakati wa Mawasiliano wakati wa maafa.
Kaimu Msemaji Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Julian Tendwa, akizungumza na waandshi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akielezea kuhusu Mapngo wa Taifa wa Kujiandaa Kukabiliana na Majanga na Mkakati wa Mawasiliano wakati wa maafa. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Habari, Maelezo, Zamaradi Kawawa na kushoto ni Ofisa Habari wa ofisi hiyo, Francisca Swai.
Kaimu Msemaji Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Julian Tendwa, akizungumza na waandshi wa habari, Dar es Salaam jana, wakati alipokuwa akielezea kuhusu Mapngo wa Taifa wa Kujiandaa Kukabiliana na Majanga na Mkakati wa Mawasiliano wakati wa maafa. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Habari, Maelezo, Zamaradi Kawawa na kushoto ni Ofisa Habari wa ofisi hiyo, Francisca Swai.
Kaimu Msemaji Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Julian Tendwa, akiwaonesha waandshi wa habari, Dar es Salaam leo, kijarida cha Mapango wa Taifa wa Kujiandaa Kukabiliana na Majanga na Mkakati wa Mawasiliano wakati wa maafa. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Habari, Maelezo, Zamaradi Kawawa.

1. Utangulizi
Ndugu
wana habari karibuni sana katika mkutano huu ambapo leo Ofisi ya Waziri Mkuu
kupitia Idara ya Uratibu wa Maafa inazungumza nanyi kuhusu Mpango wa Taifa wa
kujiandaa na Kukabiliana na Maafa na
Mkakati wa Taifa wa Mawasiliano wakati wa Maafa.
Kama
mnavyofahamu nchi yetu imekuwa ikikumbwa na majanga mbalimbali ambayo husababisha
maafa.
Maafa
hayo, yapo yanayotokana na Nguvu za Asili kama ukame, mafuriko, vimbunga,
magonjwa ya mlipuko nk. Vilevile, kuna maafa yanayosababishwa na shughuli za kibinadamu.
Mifano ya maafa hayo ni ajali za vyombo vya usafiri, Moto wa viwandani,
maofisini na majumbani nk.
Ningependa
ifahamike kuwa Maafa ni matokeo ya janga ambalo
huathiri kwa kiwango kikubwa mfumo wa kawaida wa maisha ya jamii kwa
kusababisha vifo, majeraha, upotevu au uharibifu mkubwa wa mali au mazingira ambayo jamii iliyoathirika isipokuwa
imejiandaa na maafa haiwezi kuyakabili maafa kwa uwezo au rasilimali zake bila
msaada kutoka nje ya jamii hiyo.
Kwa
kuzingatia hayo Serikali kupitia Idara
yake ya Uratibu wa Maafa imeandaa Mpango wa Taifa wa Kujiandaa na Kukabiliana
na Maafa unaoainisha majukumu ya Wadau mbalimbali, kwa ajili ya
kuhakikisha kunakuwa na ufanisi katika jamii nzima kwa kuwa na uelewa mkubwa wa
kujiandaa, kukabili na kupunguza athari za maaf nchini.
Mpango
huu pamoja na Mkakati wa Mawasiliano ilizinduliwa mwezi Novemba, 2012 na Waziri
mwenye dhamana ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia
Sera, Uratibu na Bunge Mhe. Wiliama V Lukuvi (MB) kwa wadau na
kueleza jinsi itakavyosaidia kutoa muongozo wa namna ya utekelezaji wa kuratibu
maafa katika ngazi ya Taifa.
Kama
mnavyofahamu, maafa ni suala mtambuka linalomhusu kila mmoja wetu katika
kukabiliana nalo, ambapo hata ninyi ndugu zangu wanahabari ni moja ya nguzo kuu
ya kushiriki katika kukabiliana nayo.
Katika Mpango huu pamoja na Mkakati wa
Mawasiliano vyote vimeainisha majukumu ya kila mdau ili kutambua ni upi wajibu wa mdau husika
pindi dharura ya maafa inapotokea.
Tukizingatia ushiriki huo na mfumo wetu wa kukabiliana na maafa ambao una
Kamati za Maafa kwenye ngazi ya mkoa, wilaya hadi kijiji ambazo zina majukumu
ya kusimamia masuala ya maafa katika maeneo yao. Hivyo
kila mdau ataweza kushiriki kikamilifu katika hatua zote za kujiandaa, kukabiliana na kupunguza Athari za maafa.
2. Lengo
Kama
nilivyoeleza awali, faida ya kuwa na Mpango huu pamoja na Mkakati wa
Mawasiliano ni kurahisisha uratibu wa shughuli za maafa kwa kuainisha majukumu na kuwezesha upatikanaji
wa mahitaji ya msingi wakati wa dharura na namna wadau mbalimbali watakavyo
shiriki katika shughuli za uratibu wa maafa na hatimaye kuweza kurudisha hali
ya kawaida.
Mpango
huu pamoja na Mkakati wa Mawasiliano vimeletwa kwenu Wanahabari ili ninyi
wenyewe muweze kuufahamu pamoja na kusaidia Wadau wengine na wananchi kwa
ujumla kutambua majukumu yao ili kila mmoja aweze kutekeleza wajibu wake kwa
ufanisi ili tuweze kuzuia au kupunguza athari za maafa.
Aidha
serikali kwa kupitia Idara ya Uratibu wa Maafa iliona umuhimu wa kuandaa
Mkakati wa Mawasilianao ukiwa na lengo la kuhakikisha Mpango wa Taifa wa Kujiandaa
na Kukabiliana na Maafa unatekelezeka kikamilifu. Mkakati huu utakuwa ndio Dira
ya kupata taarifa, kutoa elimu na tahadhari kwa Umma juu ya masuala yote
yanayohusu maafa na jinsi ya kujiandaa, kukabiliana nayo pindi yanapo kuwa yametokea.
Lengo
la Mpango na Mkakati huu ni kuweza kujipanga na kuwa imara katika utekelezaji
mzuri wa masuala menejimenti ya maafa na dharura zinazotokana na majanga pindi yanapokuwa yameikumba nchi yetu.
Idara
ya Uratibu wa Maafa imeona ni vyema kuja kuwaeleza wanahabari mipango iliyonayo,
hii ikiwa ni katika kuboresha mawasiliano ya Maafa pamoja na namna ya
kukabiliana na maafa na kupunguza ucheleweshwaji wa taarifa kutoka katika maeneo yalipo tokea maafa nchini.
Aidha,
napenda kuchukua nafasi hii kuwa taarifu kuwa Tarehe 13 Oktoba, 2013 ya kila
mwaka ni Siku ya Kimataifa ya Upunguzaji Athari za Maafa Duniani. Mwaka huu (tarehe
13 Oktoba, 2013) Ofisi ya Waziri Mkuu itaadhimisha siku hiyo ambapo kwa mujibu
wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Upunguzaji wa Athari za Maafa
(United Nationas International Strategy
for Disaster Risk Reduction (UNISDR) limetoa kaulimbiu isemayo ’’Ulemavu na Maafa, SUALA LISILOZUNGUMZWA
BAYANA – Tujumuike Pamoja”
“Disability and Disasters A NOT SO OBVIOUS
CONVERSATION - Join in”.
Siku
hii inaadhimishwa maalumu kila mwaka kwa kuwa na kaulimbiu yenye kutoa
kipaumbele katika suala linalohitaji kupewa mkazo katika jamii. Kwa mwaka huu
maadhimisho haya yameelekezwa katika kundi la watu wasiojiweza, yaani
Walemavu ikiwa na lengo la kuwakumbusha Wadau wote wa Maafa pamoja na jamii kwa ujumla kuwa kila mmoja ulimwenguni anahitaji
Kinga dhidi ya Maafa,vilevile masuala ya Uwekezaji, Maamuzi na maandalizi ya
Sera na mikakati ya Kupunguza Athari za Maafa yahusishe mahitaji ya makundi
maalumu, ikiwemo walemavu.
Nawashukuru
na asanteni sana kwa kunisikiliza
Imetolewa
na
KAIMU
MSEMAJI/ OFISI YA WAZIRI MKUU
02
Septemba, 2013
No comments:
Post a Comment