TANGAZO


Monday, September 2, 2013

Viongoizi wa Dini wakerwa na vitendo vya Wabunge Bungeni

Askofu wa Dayosisi ya Kati (DCT), Godfrey Muhogolo akisisitiza jambo kwa waumini wa Kanisa la Adrea Mtakatifu Anglikana lililopo Veyula, Manispaa ya Dodoma wakati alipokuwa akizindua kanisa hilo baada ya ujenzi kukamilika.
Kamati ya ujenzi wa Kanisa hilo, ikiwa mbele ya Askofu Godfrey Muhogolo, aliyewaita kuwatambulisha na kuwapongeza kutokana na kusimamia fedha vizuri zilizotumika kwa ujenzi huo.
Baadhi ya wachungaji wa Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Kati wakipewa maelekezo ya namna ya kuwalisha waumini wa kanisa hilo, waliohudhuria uzinduzi jinsi ya kuwashirikisha meza ya Bwana maarufu kama mkate.
Mwenyekiti wa Bakwata, Wilaya ya Chamwino, Sheikh akisisitiza jambo kwa waumini wa madhehebu ya Kianglikana alipokuwa amekaribishwa kujionea uwekaji wakfu wa kanisa hilo, lililopo Veyula katika Manispaa ya Dodoma.
Mwenyekiti wa Bakwata Wilaya ya Chamwino akizungumza na waumini wa Dhehebu la Kianglikana wakati wa Ibada ya uzinduzi wa Kanisa hilo, uliofanyika Veyula chini ya Askofu Godfrey Muhogolo.
Waumini wa Kanisa la Andrea Mtakatifu Anglikana wakiwa ndani ya kanisa hilo, wakati wa uzinduzi wa kanisa hilo, lililojengwa kwa gharama ya zaidi ya sh. mil. 194. (Picha zote naJohn Banda

Na John Banda, Dodoma
VIONGOZI wa madhehebu ya dini, wanaendelea kukerwa na vituko mbalimbali vikiwemo mipasho na hata kutishia kupigana ambavyo vimekuwa vikioneshwa na baadhi ya Wabunge katika vipindi vya Bunge mjini Dodoma.

Viongozi hao walionyesha hisia za kero hizo mbele ya waumini wa kanisa la Andrea Mtakatifu Anglikana Paleshi ya Veyula walipohudhuria uzinduzi wa jingo la kuabudia lililopo katika kijiji hicho leo, Kata ya Makutupora, Manispaa ya Dodoma.

Askofu wa Anglikan Dayosisi ya kati (DCT), Godfrey Mdimi Muhogolo alisema wabunge wamechaguliwa na wananchi kutokana na kuaminiwa sasa inashangaza kuona kuwa badala ya kufanya uwakilishi waliotumwa wanageuka kuwa wapashanaji, kutukanana na kutishiana.

Muhogolo alisema wananchi wanakuwa na matumaini ya changamoto na yote wanayowatuma wabunge yafikishwe bungeni ili ikiwezekana serekali iyafanyie kazi badala yake inakuwa kinyume bunge linageuzwa kuwa majukwaa ya siasa na ulingo wa masumbwi ambayo kabla ya wahusika kupigana huanza kwa kutambiana.

Aliongeza kuwa wabunge waliochaguliwa na wananchi ni wasomi kuliko mabunge yaliyotangulia hivyo kama wao wakianzisha fujo bungeni wananchi wao itakuwaje majimboni mwao na cha kusikitisha zaidi wengi wao ni vijana wenye nguvu wanaotegemewa sana na Taifa hili.

“Mimi kama askofu naona hayo yote yanatokana na ukosefu wa hekima, Busara na maadili na ni ngumu kuendesha nchi kwa kutumia nguvu badala ya hoja, usomi wote ni bure hasa kwa vijana heshima ya mtu haipotezwi na Siasa kila mtu afanye wajibu wake ipasavyo ili kurudisha imani ya watanzani kwenye Bunge lake’’, alisema Muhogolo.

Naye Mwenyekiti wa Bakwata Wilaya ya Chamwino Shekh Said Abubakar Gantana mualikwa katika uzinduzi huo wa kanisa alisema Vitendo hivyo vya kubishana na kutukanana ni vya aibu kwa watanzania na pia kuaibisha viaongozi wao wa Dini kutokana na wabunge wote kushiriki kwenye madhehebu mbalimbali.

Aliwataka wabunge na uongozi mzima wa Bunge kuiga mfano wa viongozi wa Dini ambao wamekuwa wakishirikiana katika mambo mbalimbali katika jamii ili kuendelea kuijenga amani na kuimalisha umoja wa kitaifa uliojengwa na waasisi wa nchi hii waliotangulia akiwemo Hayati Nyerere.

Jengo hilo la kanisa, nyumba ya utumishi,Vyoo Pamoja na samani vimigharim zaidi ya 194 MIL walizolipwa ili kupisha mradi wa Barabara ya Dodoma Arusha unaoendelea kwa kiwango cha lami.

Katibu wa kamati ya ujenzi Marry Nghambala alisema walitumia 173,537,950 kujengea na kununua samani za kanisa, ujenzi wa nyumba ya utumishi ambayo haijakamilika ilitumia 14,466,100 na ujenzi wa vyoo na nyumba za uani kwenye nyumba ya utmishi 6,730,100 na jumla yake ikiwa 194, 734, 150.

No comments:

Post a Comment