Malkia kutoka katika falme za kiafrika wanakutana mjini Kampala kujadili nyenzo za kupigana dhidi ya mila na tamaduni zenye madhara kwa wanawake.
Mkutano huo unaoandaliwa na malkia wawili wa Uganda , pia utajadili swala la haki za wanawake.
Malkia hao wa kiafrika pamoja na mtandao wa viongozi wanawake wa kitamaduni Afrika unaofadhiliwa na Umoja wa Mataifa utazinduliwa rasmi kwenye mkutano huo
Mataifa mengi ya Afrika bado yapo na wafalme wa kitamaduni mfano Ghana, Uganda na Swaziland.
Baadhi ya tamaduni na mila zinazoathiri wanawake pakubwa sana Afrika ni pamoja na ndoa za mapema, ukeketaji na ndoa za kulazimishwa
No comments:
Post a Comment