TANGAZO


Monday, September 2, 2013

Makumbusho ya Kimila yaliyopo Mlima Bwibwi yalivyobomolewa na CDA, mkoani Dodoma

Mbuge wa Dodoma Mjini Dk. David Malole ambae ni mjumbe wa Bodi ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA), akionyeshwa miti na mabaki mengine na Mtemi Lazaro Chihoma namna Makumbusho hayo ya kimila yaliyojengwa katika mlima wa Bwibwi yalivyobomolewa na CDA.
Mjumbe wa Kamati ya siasa CCM Wilaya ya Dodoma Judith Myeya akifafanua jambo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mala baada ya kujionea jinsi makumbusho ya kimila ya kabila la kigogo yalivyobomolewa na Mamlaka ya ustawishaji makao makuu CDA, na kupendekeza mamlaka hiyo ifutwe.
Mtemi Lazaro Chihoma Akiwaonyesha baadhi ya watu wakiwemo Mbunge wajimbo la Dodoma mjini Dk. David Malole na wa CCM waliofika kuona jinsi makumbusho hayo ya kimila yalivyovunjwa na CDA.
Chief Lazaro chihoma (katikati), akiwaongoza Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Dk. David Malole, Katibu Mwenezi wa CCM wilaya Salum Kalli, mjumbe wa ya siasa wa wilaya CCM, Judith Myeya na viongozi wengine kuona sehemu ya Ikulu ya kimila ilivyohalibiwa na CDA.
Wananchi wa kijiji cha Iyumbu wakiwa wamejiinamia wasijue la kufanya baada ya tinga tinga la CDA kufika na kubomoa Makumbusho ya kimila yaliyojengwa katika mlima wa Bwibwi chini ya ulinzi mkali wa polisi mwishoni mwa wiki.
Mjumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Usitawishaji Makao Makuu (CDA), Dk. David Malole akijadiliana jambo na Mtemi wa kabila la Kigogo Lazaro Chihoma (kulia) na Mzenge Tumbi Andason Chaulema kwenye makumbusho ya kimila yalibomolewa na Tinga tinga la CDA chini ya ulinzi mkali wa Polisi.
Nyama za mbuzi na ngombe ni bidhaa pekee inayochangamkiwa sana na wananchi wa ndani na nje ya Mkoa wa Dodoma wakiwemo Wabunge katika Mnada unaofanyika kila siku ya Jumamosi uliopo Msalato, mkoani Dodoma. Wachomaji hawa walinaswa wakiwa kazini mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mtemi wa Makumbusho ya Kimila, Lazaro Chihoma akitoa tangazo la kuendelea na ujenzi kwa mara nyingine mbele ya waandishi wa habari siku moja tangu makumbusho hayo, yaliyopo katika Mlima wa Bwibwi kubomolewa na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA), mwishoni mwa wiki.
Mmoja wa wananchi wa kijiji cha Iyumbu akiendelea na ujenzi wa moja ya nyumba za matambiko ya kimila kwa kabila la kigogo siku moja baada ya CDA kufika na kubomoa nyumba hizo zilizojengwa kwa miti juu na chini bila kujali kisima chenye kumbukumbu za kihistoria kilichopo katika eneo hilo. (Picha zote na John Banda)

No comments:

Post a Comment