Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Rasilimali Profesa Marten Victor (kushoto), akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani), jinsi mradi wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu (STHEP), ulivyotekelezwa kwa ushirikiano wa Serikali na Bank ya Dunia, Utakavyoongeza ufanisi wa chuo hicho. Kulia ni Msimamizi wa Mradi wa Bank ya Dunia unaotekelezwa katika chuo hicho, Shaaban Mbogo.
Mratibu wa Mradi wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu (STHEP), kitaifa, Dk. Keneth Hosea (kushoto), akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), jinisi mradi huo utakavyo wanufaisha walimu wa shule za Sekondari wenye shahada wanaofundisha masomo ya sekondari. Kulia ni Msimamizi wa Mradi wa Bank ya Dunia unaotekelezwa katika chuo hicho, Shaaban Mbogo.
Mhandisi John Kapuku akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani), Jengo la Sayansi ya Majini na Teknolojia ambayo ni moja ya jengo, linalotokana na mradi huo unaofadhiliwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Bank ya Dunia, lililogharimu bilioni 4.3.
Jengo la Urithi wa Utamaduni, linalotokana na mradi huo, unaofadhiliwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Bank ya Dunia, lililogharimu bilioni 2.6.
Jengo la Uhandisi Migodi
linalotokana na mradi huo unaofadhiliwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Bank ya Dunia lililogharimu bilioni 2.8. (Picha zote na Hassan Silayo-Maelezo)
KATIKA kukabiliana na changamoto zinazoikabili Elimu ya Juu nchini, Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi inatekeleza Mradi wa Sayansi,
Teknolojia na Elimu ya Juu (Science Technology and Higher Education
Project - STHEP) ambao unafadhiliwa na Benki ya Dunia. Mradi huu umejikita katika nyanja kuu 4 ambazo ni: kuboresha
rasilimali watu kwa kutoa mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi (staff
development), kujenga, kupanua na kukarabati vyumba vya mihadhara, maktaba, maabara na karakana (Civil Works), kununua
vifaa vya kufundishia vikiwemo vifaa vya maabara na TEHAMA, vitabu na magari (Procurement of Goods) na kuboresha mitaala, sera na usimamizi kwa kutumia
wataalamu washauri (Consultancy services for curriculum review, policy,
capacity building, design and supervision of civil works).
Taasisi
15 za umma zinazotekeleza mradi huu ni Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT),
Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU), Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA), Taasisi ya Teknolojia
Dar es Salaam (DIT), Chuo Kikuu Kishiriki cha Ualimu Dar es Salaam (DUCE), Chuo
Kikuu Kishiriki cha Ualimu Mkwawa (MUCE), Chuo Kikuu cha Dares Salaam (UDSM),
Chuo Kikuu cha Serikali cha Zanzibar (SUZA).
Taasisi
nyingine ni Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), Baraza
la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bodi ya Mikopo
ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
(MCST) na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Hadi
sasa Mradi umegharamia mafunzo ya muda mrefu kwa watumishi 191 wa taasisi za umma masomo ya Shahada
ya Uzamivu (PHD) na watumishi 208 wamepata ufadhiri wa mafunzo ya Shahada za Uzamili
(Masters) katika fani za sayansi, teknolojia na ualimu. Aslilimia 30 ya watumishi
hawa wanasomeshwa katika vyuo vikuu bora katika nchi zilizoendelea ikiwemo Uingereza,
asilimia 30 wanasomeshwa katika nchi zinazoendelea mfano Afrika Kusini na kwingineko
na waliobaki (asilimia 40) wanasomeshwa hapa nchini. Asilimia 15 ya watumishi
wanaosomeshwa na mradi huu wamekamilisha masomo yao na wengine watamaliza
mwishoni mwa mwaka huu. Vilevile watumishi 467 wamesomeshwa mafunzo maalum ya
muda mfupi.
Aidha,
mradi umejenga jumla ya majengo 25 ya mihadhara, maktaba, ofisi na karakana ambapo mengi yapo kwenye hatua za mwisho
kukamilika katika taasisi mbalimbali.
Majengo
haya yatatumiwa na jumla ya wanafunzi 36,344 wa elimu ya juu na wakufunzi na wahadhiri
1,640 katika taasisi za ARU, DUCE, DIT, OUT, MUCE, SUA na UDSM.
Mradi
huu pia umenunua vifaa vya kufundishia na kujifunzia vikiwemo vifaa vya maabara,
vifaa vya TEHAMA 1,831, vitabu 4,598, mitambo ya kufundishia na magari 19.
Mradi wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu umesaidia
Tume ya Vyuo Vikuu kujenga uwezo wa
TEHAMA na kuwezesha kudahili wanafunzi wote wanaojiunga na elimu ya juu kwa pamoja
(Central Admissions System - CAS) na umeiwezesha TCU kutoa mwongozo wa ubora wa Vyuo Vikuu hapa
nchini (Universities Standards and Benchmarks).
Aidha,
mradi umewezesha Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kuandaa miundombinu
ya TEHAMA ili waombaji wa mikopo ya Elimu ya juu waombe kwa kutumia mtandao (Online
Loan Application System - OLAS).
Mradi wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu pia umesaidia
TCU kujenga uwezo wa kukokotoa ada elekezi kwaajili ya wanafunzi wa elimu ya juu
(Higher Education Students Unit Cost).
Mradi
wa STHEP ni wa muda wa miaka 7 ukiwa na duru mbili ziitwazo Adaptable Lending Program-1 (APL-1) na Adaptable Lending Program–II (APL-II).
Duru ya kwanza ilianza Julai 2008.
Duru ya pili inatazamiwa kuanza kabla ya duru
ya kwanza kuisha hapo Desemba, 2013 na kukamilika June, 2016.
Mradi huu unalenga kuongeza
matumizi ya taaluma katika shughuli za kiuchumi nchini (application of
knowledge in economic activities), na malengo ya haraka (immediate goal)
yakiwa ni kuongeza idadi ya wanafunzi na kuboresha mazingira ya kufundishia
katika elimu ya juu hapa nchini kipaumbele kikiwa katika fani za sayansi,teknolojia
na ualimu.
Ntambi
Bunyazu
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini
No comments:
Post a Comment