TANGAZO


Sunday, September 1, 2013

Kambi Kazi ya Vijana wa Mbelei, Halmashauri ya Bumbuli kupitia Programu ya TAYODEA yafungwa rasmi


Jengo la Kituo cha vijana wa Kijiji cha Mbelei kilichopo Kata ya Mamba katika Halmashauri ya Mji wa 
Bumbuli lililojengwa na 
vijana 14 waliokuwa kambini 
kwa siku 21 saba wakiwa ni watanzania na saba
Wajerumani na wengine watano waliokuwa 
wakishiriki ujenzi huo linavyoonekana katika awamu 
ya kwanza ya ujenzi uliogharimu sh.milioni 9. Jengo 
hilo ambalo litaanza kutumika January mwakani 
litagharimu zaidi ya sh.milioni 60 
likikamilika kitakuwa Kituo cha habari cha vijana 
(Youth Resource Centre), kwa vijana 
wa kata hiyo na vijiji jirani.


Raia wa Ujerumani walioshiriki ujenzi huo wakisoma gazeti wakati wa hafla ya kufunga kambi hiyo 
iliyofungwa Agosti 30, 2013 katika kijiji 
cha Mbelei.


Mkurugenzi Mtendaji wa TAYODEA Mkoa wa Tanga, David Chanyeghea (kushoto), akimuongoza 
mgeni rasmi aliyefunga kambi hiyo kwa niaba wa 
Ofisa Tawala wa Mkoa wa Tanga, Donald Makawia 
(katikati) na Diwani wa Kata ya Mamba Zubeda Titu 
kukagua jengo hilo.
Wazee wa Kijiji cha Mbelei wakiwa kwenye hafla hiyo.


Mkurugenzi Mtendaji wa TAYODEA Mkoa wa Tanga, David Chanyeghea (katikati), akimuelekeza jambo 
mgeni rasmi aliyefunga kambi hiyo kwa niaba wa 
Ofisa Tawala wa Mkoa wa Tanga, Donald Makawia 
wakati akikagua jengo hilo. Kushoto ni Diwani wa 
Kata ya Mamba Zubeda Titu. 


Wananchi wa Kijiji cha Mbeleiu,  vijana wa TAYODEA na Raia wa Ujerumani wakiwa kwenye hafla hiyo.


Mkurugenzi Mtendaji wa TAYODEA Mkoa wa Tanga, David Chanyeghea (wa pili kushoto), mgeni rasmi 
Donald Makwaia (katikati), Diwani wa Kata ya 
Mamba Zubeda Tituy na Makamu Mwenyekiti wa 
Halmashauri ya Mji wa Bumbuli, Bakari Kavumo 
(kushoto), wakiwa kwenye hafla hiyo.


Raia wa Ujerumani walioshiriki katika kambi kazi hiyo.




Wakina mama wa Kijiji cha Mbelei wakiwa kwenye hafla hiyo.


Wananchi wa Kijiji cha Mbelei na Raia wa Kijerumani 
wakiwa wamekaa mbele ya jengo linalojengwa kwa 
ajili ya kituo cha habari cha vijana.




Wakazi wa Kijiji cha Mbelei wakiwa kwenye sherehe  za kufunga kambi hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa TAYODEA Mkoa wa Tanga, David Chanyeghea (kushoto), akitoa taarifa fupi 
kwa mgeni rasmi ya ujenzi wa kituo hicho.

Washiriki wa kambi hiyo wakiimba wimbo wa Tanzania nakupenda huku wakiwa wameshikana mabegani ikiwa 
ni ishara ya mshikamano.

Mgeni rasmi Donald Makwaia akimpongeza kiongozi wa msafara wa raia wa Ujerumani 
Jonas Scha'nemann kwa kuchaguliwa kuwa baba wa 
kambi hiyo kwa mwaka 2013 (Mr Camp 2013).

Mkurugenzi Mtendaji wa TAYODEA Mkoa wa Tanga, 
David Chanyeghea  akimpongeza  raia wa Ujerumani 
Miriam Kroschewski kwa kuchaguliwa kuwa mama 
wa kambi hiyo kwa mwaka 2013 (Miss Camp 2013)

Miss Camp 2013 Miriam Kroschewski na Mr Camp 2013 Jonas Scha'nemann wakiwa katika 
picha ya pamoja.

Mgeni rasmi Donald Makwaia akikabidhi vyeti vya ushiriki katika kambi hiyo.


Mgeni rasmi Donald Makwaia akihutubia wakati akifunga
 kambi hiyo.
Raia wa Ujerumani wakimkabidhi mpira na jezi Mkurugenzi Mtendaji wa TAYODEA David Chanyeghea 
kwa ajili ya vijana wa Kijiji cha Mbelei na Kata ya Mamba.

Mgeni rasmi Donald Makwaia akimkabidhi mpira 
Mwenyekiti wa vijana wa Kata ya Mamba aliyefahamika 
kwa jina moja la Shedangio. Mpira huo na jezi vilitolewa 
na raia wa Ujerumani walioshiriki kambi hiyo.

Mkurugenzi wa TAYODEA Mkoa wa Tanga, David Chanyeghea (katikati), akizungumza na vijana wa TAYODEA walioshiriki kambi hiyo.

Raia saba wa Ujerumani walioshiriki kambi hiyo, wakiwa katika picha ya pamoja.

Raia saba wa Ujerumani walioshiriki katika kambi hiyo, 
 wakiwa na vijana wa Kijiji cha Mbelei walioshiriki pia 
katika kambi kazi hiyo.

No comments:

Post a Comment