Wakala wa Mbegu za Miti
(Tanzania Tree Seed Agency
–TTSA
UANZISHWAJI, MAFANIKIO NA
CHANGAMOTO
Ludovick Uronu
Kaimu Mtendaji Mkuu
Wakala wa Mbegu za Miti
Mada iliyotolewa kwa waandishi
wa habari Dar es Salaam, 29 Agosti 2013
- UTANGULIZI
1.1 HISTORIA YA UANZISHWAJI WA
WAKALA WA MBEGU ZA MITI TANZANIA
1.1.1Hali
ya misitu Tanzania
Eneo lote la misitu Tanzania ni Hekta 48 millioni (Ekari 119 millioni), kati ya hizo 96% ni msitu mataji wazi (woodland),
0.3% ni misitu ya mikoko (mangrove) na 3.4% ni misitu mingineyo.
Katika eneo lote la misitu ni 33%
tu ndiyo zipo katika hifadhi ya misitu kisheria. Uharibifu wa misitu Tanzania unakadiriwa kuwa
hekta 412,000 kwa mwaka. Uharibifu huu unatokana na ukataji
wa miti kiholela ,uchomaji moto ovyo wa misitu, idadi ya mifugo inayozidi uwezo
wa eneo ,Kilimo cha kuhamahama, maendeleo ya viwanda na ujenzi wa makazi .
Athari zinazotokana na upungufu wa misitu ni: kusababisha mmmomonyoko wa udongo, uchafuzi wa hewa na
maji, kuongezeka kwa joto la dunia na upungufu wa mazao ya misitu. Ukarabati
wa maeneo ya misitu yaliypharibika unakisiwa kuhitaji takribani miche ya miti milioni
440 kwa mwaka sawa na wastani wa tani 40 ya mbegu za miti kwa mwaka
1.1.2 Historia fupi ya uzalishaji
wa mbegu za miti Tanzania
v Uzalishaji ulianza wakati
wa utawala wa Mjerumani chini ya Taasisi ya Kibaiyolojia na Kilimo iliyokuwa
imeanzishwa na Wajerumani mwaka 1902 huko Amani Mkoa wa Tanga
v Mbegu za wakati huo
zilikuwa ni aina ya Misindano (Pinus spp.), Misanduku (Cupressus spp.)
na Mikaratusi (Eucalyptus spp.)
v Mwaka 1951 serikali
ilianzisha kituo cha Utafiti wa Misitu (Silviculture Research Station) huko
Lushoto, mkoa wa Tanga mwaka 1951.
v Kituo hicho kilikuwa na
kitengo cha mbegu za miti kilianzishwa kwa madhumuni ya kuzalisha na kusambaza
mbegu za miti kwa ajili ya utafiti na mashamba ya miti ya serikali.
v Miaka ya 1970 serikali ya
Tanzania ilianzisha mpango wa kitaifa wa kupanda miti ili kuboresha mazingira
ambayo yalikuwa yameharibika pamoja na mahitaji mengine
v Kituo cha Utafiti wa
Misitu Lushoto, hakikuweza tena kumudu mahitaji hayo kwa sababu ya kijiografia
(kiko pembezoni mwa nchi, mbali na wateja wa mbegu) pia hakikuwa na vitendea
kazi vya kutosha.
v Serikali ya Tanzania ilitambua changamoto hiyo
na ndipo ilibuni Mradi wa Taifa wa Mbegu za Miti (National Tree Seed Programme
– NTSP), chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii mwaka 1989 wenye makao makuu
mjini Morogoro.
v NTSP ilikuwa na majukumu
ya kuzalisha na kusambaza mbegu bora za miti ili kukidhi mahitaji ya humu
nchini na kuuza ziada nchi za nje
v Kufuatana na programu ya
serikali ya kuboresha utumishi wa umma (Public Service reforms programme), NTSP
ilibadilishwa kuwa Wakala wa Mbegu za Miti (Tanzania Tree Seed Agency – TTSA).
- WAKALA WA MBEGU ZA MITI
TTSA yenye makao makuu yake mjini Morogoro, ni
Wakala wa Serikali unaofanya shughuli zake chini ya Wizara ya Maliasili na
Utalii. TTSA ilizinduliwa tarehe 24 Januari 2003 chini ya sheria ya Wakala za
Serikali Na. 30 ya mwaka 1997. Madhumuni
ya TTSA ni ‘’Kuwezesha upatikanaji endelevu wa mazao ya misitu
na utunzaji wa mazingira nchini kwa kuzalisha na kusambaza mbegu bora za miti
pamoja na vipandikizi vingine”.
2.1Vyanzo vya mapato vya TTSA
2.1.1
Mbegu za miti
Chanzo kikubwa cha mapato ya TTSA ni kuuza mbegu
bora za miti.TTSA inakusanya na kuuza mbegu bora za miti ndani na nje ya nchi.
Wastani wa tani 12.5 ukusanywa na kuuzwa kila mwaka ndani na nje ya nchi. Nje
ya nchi TTSA inauza mbegu za miti katika nchi za Msumbiji, Afrika Kusini,
India, Vietnam, Guatemala, Rwanda, Uganda, Australia, Botswana, Singapore ,
Ufaransa, Marekani, Madagascar, Siera leone, Denmark, Costa Rica na Malawi.
Aina
za mbegu za miti zilnazouzwa ni 195 na kati ya
hizo, aina za miti ya kienyeji ni asilimia 60 iliyosalia
ni mbegu za miti ya kigeni. Mbegu
zinazoongoza kwa kupendwa katika soko ni Mkangazi (Khaya anthotheca), Mtiki (Tectona
grandis), Mwerezi (Cedrela odorata),
Mkenge (Albizia lebbeck), na Mkongo (Afzelia quanzensis), Msindano (Pinus patula), Mtikivuli (Acrocarpus fraxinifolius).
2,1.2
Miche ya miti
TTSA inazalisha na kuuza miche ya miti kwa ajili ya
matumizi mbalimbakama mbao, nguzo, mkaa, kuni, madawa, mapambo, kilimo mseto,
kivuli na hifadhi ya maji. Pia TTSA inazalisha miche bora ya miembe na
michungwa ambayo inazaa matunda kati ya miaka miwili hadi mitatu baada ya
kupandwa. Aina ya miembe inayozalishwa ni Tommy Atkin, Kent, Keitt, Red Indian,
Dodo, Sensation, Alphonso, Apple na Julie. Aina za michungwa ni Valencia,
Parson brown, Matombo sweet, Jaffa na Orlando.
2.1.3 Kumbi za mikutano
Wakala unazo kumbi tatu za mikutano ambazo zinakodishwa,
taasisi za serikali ndio wateja wakubwa kutokana na kumbi hizo kuwa katika
mazingira mazuri na ya utulivu na uwepo wa “standby
generator”.
2.1.4
Mafunzo ya muda mfupi
Wakala unaendesha mafunzo ya muda mfupi ya uanzishaji
na uendelezaji wa bustani ya miche ya miti mara mbili kila mwaka, Aprili na Oktoba.
2.1.5
Ushauri wa kitaalamu (Consultancy)
Wakala unatoa ushauri wa kitaalamu katika Nyanja
mbalimbali za misitu, kama utambuzi wa
mimea, kuboresha mazingira (Landscaping) na kukarabati maeneo ya misitu
yaliyoharibiwa (Forest rehabilitation).
3. MAFANIKIO NA CHANGAMOTO
3.1 Mafanikio
3.1.1 Kiasi cha mbegu
na miche iliyosambazwa humu nchini
Mwaka
|
Kiasi cha mbegu (kg)
|
Idadi ya miche
|
2003
|
7,250
|
9,750
|
2004
|
8,300
|
10,150
|
2005
|
11,252
|
12,852
|
2006
|
9,587
|
32,215
|
2007
|
10,165
|
41,698
|
2008
|
9,637
|
179,670
|
2009
|
10,136
|
194,619
|
2010
|
12,300
|
61,780
|
2011
|
12.400
|
64.200
|
2012
|
3,954
|
47,016
|
2013
|
20,245
|
38,772
|
Jumla
|
102,838
|
628,586
|
Kiasi cha mbegu na
miche iliyosambazwa na TTSA katika kipindi cha miaka 10 (2003 – 2013) kinaweza
kwa wastani kutosha kupanda Ha 643,131 (Ekari 1,588,534) za misitu. Kwahiyo ufanisi wa TTSA hauwezi kupimwa kwa mapato
pekee bali kwa kiasi inachochangia katika kuboresha mazingira nchini. TTSA ni moja kati ya Wakala za serikali ambazo
zinatoa huduma na kufanya biashara.
3.2.1
Mapato na
“Sustainability” katika kipindi cha miaka kumi (2003 – 2013)
Mwaka
|
Mapato ya TTSA
|
Mchango wa Serikali (PE + OC)
|
Jumla
|
TTSA Sustainability
|
2003/2004
|
131,621,570
|
322,245,913
|
453,867,483
|
29%
|
2004/2005
|
182,280,991
|
405,722,206
|
588,003,197
|
31%
|
2005/2006
|
245,896,401
|
328,858,095
|
574,748,496
|
43%
|
2006/2007
|
359,422,408
|
315,359,104
|
674,781,512
|
53%
|
2007/2008
|
327,906,170
|
320,210,671
|
648,116,841
|
51%
|
2008/2009
|
337,067,686
|
453,664,265
|
790,731,951
|
43%
|
2009/2010
|
426,169,954
|
453,203,302
|
879,373,256
|
48%
|
2010/2011
|
338,574,949
|
589,186,785
|
927,761,734
|
36%
|
2011/2012
|
186,736,420
|
579,419,000
|
766,155,420
|
24%
|
2012/2013
|
472,144,267
|
499,676,110
|
971,820,377
|
49%
|
3.1.3 Vyanzo
vya mbegu bora
TTSA ina
vyanzo 385 vya mbegu. Vyanzo hivyo vipo maeneo mbalimbali ikiwemo katika
hifadhi za misitu. TTSA imeendelea kuboresha vyanzo vya mbegu pamoja na
kuanzisha vyanzo vipya vya mbegu kutokana na mbegu zilizoboresha ili kuendelea
kupata mbegu bora zaidi.
Baadhi ya
vyanzo vya mbegu vilivyoboreshwa ni:Mtiki (Tectona
grandis),Msindano (Pinus patula),
Mkaratusi (Eucalyptus grandis),Mkaratusi
(Eucalyptus tereticornis), Mkorimbia
(Corymbia citriodora,)Mgrevilea (Grevillea robusta),Mvule (Milicia excelsa), Mninga (Pterocarpus angolensis),Mwarobaini (Azadirachta indica), Mtiki mweupe (Gmelina arborea,)na Mgliricidia (Gliricidia sepium).
3.1.4 Mafunzo
mafupi ya Uanzishaji na Uendelezaji wa Bustani ya vitalu vya miti
Katika
kipindi cha miaka 10 TTSA imetoa mafunzo mafupi ya uanzishaji na uenelezaji wa
bustani za vitalu vya miti kwa washiriki 400 katika mikoa ya Arusha, Dodoma,
Dar es Salaam, Iringa, Morogoro, Kilimanjaro, Mtwara, Pwani, Mara, Mwanza,
Tanga, Kigoma, Tabora, Singida, Shinyanga, Pemba na Unguja.
3.1.5 Ushauri wa kitaalamu (Consultancy)
TTSA
imetoa ushauri wa kitaalamu wa tambuzi wa mimie ya aslili na ushauri wa mimea
ya kuboresha mazingira (Rehabilitation) katika makampuni manne ya migodi ya
dhahabu ya Geita Gold Mine, Tulaweaka Gold Mine, Resolute Tanzania na North Mara
Gold Mine pia Kiwanda cha Cement Tanga. Pia imetoa ushauri wa uanzishaji na
uendelezaji wa bustani za vitalu vya miche kwa wadau mbalimbali wa miradi ya
upandaji miti.
3.1.5 Ajira
TTSA
imefanikiwa kuajiri jumla ya watumishi 30 wapya wa kada mbalimbali mara mbili
baada ya kupata kibali cha ajira.
3.1.7 Wafanyakazi
waliojiendeleza kielimu
Tangu
2003 hadi 2013 TTSA ilipoanzishwa baadhi ya wafanyakazi wamejiendeleza kielimu
na wakahitimu katika ngazi mbalimbali kama ifuatavyo:
·
PhD
(Biology) ---------------------------------- 1
·
MSc.
(Forestry) ------------------------------- 1
·
MSc.
(Seed Conservation) ----------------- 1
·
BSc.
(Forestry) -------------------------------- 2
·
BA (Human
Resource) ---------------------- 1
·
Adv.
Diploma (IT) ----------------------------- 1
·
Diploma
(Secretarial Studies) ------------- 1
·
Certificate
(Forestry) ------------------------- 6
3.1.8 Wafanyakazi walioko
masomoni ni kama ifuatavyo:
·
MBA
(Human Resource) ------------------- 1
·
MAB
(Corporate Management)-------------- 1
·
BSc.
(Forestry) -------------------------------- 2
·
Bachelor
Degree (Accoutancy)------------- 1
·
BSc.
(Lab. Science) -------------------------- 1
·
Diploma
(Forestry------------------------------- 1
3.1.8
Wadau wanaofaidika moja kwa moja na huduma za TTSA:
Miradi ya serikali
inayojihusisha na upandaji miti
Mashirika ya siyo ya
kiserikali yanayojihusisha na upandaji miti
Halmashauri za Wilaya,
Mashamba ya miti ya
wawekezaji
Watu binafsi wenye
bustani za miche,
Wanavijiji na
wakulima.
3.1.9 Ushirikiswaji wa umma
v Karibu ya 1/3 ya mashamba
ya mbegu ya TTSA yapo katika ardhi inayomilikiwa na wananchi.
v Mbegu zinazokusanywa
hatimaye husambazwa kwa wananchi kupitia wakala za serikali na mashirika yasiyo
ya kuserikali ambao ni wateja wa TTSA.
v Wananchi wanashirikishwa
katika ukusanyaji wa baadhi ya mbegu za miti chini ya usimamizi wa wataalamu wa
TTSA na hulipwa kwa kazi hiyo. Hivyo hupata pesa na kuboresha maisha yao.
3.2 CHANGAMOTO NA UFUMBUZI WAKE
3.2.1 Upungufu wa Wafanyakazi
- TTSA inawafanyakazi 53 tu
ukilinganisha na 128 ambao ndio wanaotakiwa.
- Kila
mwaka TTSA inaajiri watumishi wapya baada ya kupata kibali kutoka
serikalini.
- Ni matumaini yetu
kuwa miaka michache ijayo wakala utakuwa na watumishi wa kutosha.
- TTSA inatarajia
kushirikiana na watu wenye maduka ya pembejeo za kilimo kusambaza mbegu
kwa kutumia vifuko vidogo.
3.2.2 TTSA
ni ndogo
v TTSAS ni ndogo sana
ukilinganisha na ukubwa wa nchi yetu.
v Tunayo mpango wa
kuanzisha kituo cha nne cha Kanda ya Ziwa huko katika jiji la Mwanza kwa ajili
ya kuhudumia mikoa mitano inayozunguka ziwaVictoria.
v TTSA inafanya mchakato
wa kuchagua watu binafsi wa kusambaza mbegu za miti katika mikoa sita.
v TTSA inatarajia
kuwatumia watu hao kusambaza mbegu kwa kutumia vifuko vidogo.
v TTSA inashirikiana na
Chuo Kikuu cha Copenhagen katika mpango huu wakutumia vifuko vidogo.
3.2.3 Uwezo mdogo wa wateja
v Wateja walio wengi wana
uwezo mdogo kifedha hivyo wanalalamika kuwa bei za mbegu ni kubwa.
v TTSA inajitahidi
kutoongeza bei za mbegu.
v Kuuza mbegu katika
mifuko midogo kutapunguza tatizo hili kwa kiasi.
3.2.4 Kutojulikana sawasawa
v Watu wengi bado hawajui
kuwepo kwa TTSA.
v Mkakati wa TTSA ni
kujitangaza katika vyombo vya habari (magazeti, radio, vipeperushi, TV, mabango
n.k)
v Pia tunatembelea wateja
wetu mara kwa mara na kushiriki katika maonyesho ya kimataifa sabasaba na
kitaifa nanenane.
3.2.4 Mchango mdogo kutoka serikalini
- Kila mwaka TTSA
inapoandaa bajeti hushauriwa na serikali iipunguze.
- Kuna miaka ambapo
pesa zilizoidhinishwa hazitolewi zote.
- Hili ni eneo
mojawapo ambalo tunahitaji wahisani.
4. MAJUMUHISHO
- TTSA inajivunia
kuwa na mazingira mazuri ya kufanyia kazi. Pia serikali huwa inateua Bodi
ya Ushauri (Ministerial Advisory Board-MAB) yenye Mwenyekiti na wajumbe
wenye busara ambao wanateuliwa na Waziri wa Maliasili na Utalii. TTSA pia
ina wafanyakazi mahiri wenye taaluma zinazotakiwa, wanaojituma na
kuwajibika.
- Hii ndiyo maana
TTSA ni mojawapo ya taasisi bora za mbegu za miti katika Afrika.
No comments:
Post a Comment