Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Bibi Mizinga (kulia) na Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Bibi Mwinda Kiula Mfugale (kushoto), wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ilyosomwa kwa niaba yake na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Profesa Elisante Ole Gabriel (hayupo pichani), alipokuwa akiyafungua mafunzo ya siku mbili kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Benjamin William Mkapa leo, jijini Dar es Salaam. Mafunzo hayao yanalenga kumjengea kijana tabia ya kujiwekea akiba ikiwa ni njia ya kumfanya aweze kujitegemea.
Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Bibi Mwinda Kiula Mfugale, akielezea jambo kwa waandishi wa habari kuhusu mpango wa NBC benki kutoa mafunzo kwa wanafunzi juu ya umuhimu wa kuweka akiba kwa manufaa ya baadaye. NBC inaendesha mafunzo kwa vijana walioko mashuleni nchini kote ambapo mpango huo wameupa jina la 'VIJANA LEO NA KESHO'
Meneja Mkuu wa Masuala ya Jamii kutoka benki ya NBC, akitoa mada kuhusu namna ya kuweka akiba kwa manufaa ya baadaye kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Benjamin William Mkapa leo, jijini jijini Dar es Salaam.
Meneja Mkuu wa Masuala ya Jamii kutoka benki ya NBC akitoa mada kuhusu namna ya kuweka akiba kwa manufaa ya baadaye kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Benjamin William Mkapa leo, jijini jijini Darc es Salaam.
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Benjamin William Mkapa akichangia mada wakati wa mafunzo kuhusu umuhimu wa kuweka akiba benki, mafunzo ambayo wanafunzi hao wanawezeshwa na wafanyakazi wa benki ya NBC.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel mwenye suti nyeusi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzo ya umuhimu wa kuweka akiba benki mafunzo ambayo yanaendeshwa na wafanyakazi wa benki ya NBC kote nchini. Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Bibi Mwinda Kiula Mfugale, Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Bibi Mizinga Melu. Kutoka kushoto ni Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Benjamini William Mkapa, Mwalimu Shanina Athman na Mkuu wa Shule hiyo, Gebo Steven Lugano. (Picha zote na Idara ya Habari, Maelezo)
No comments:
Post a Comment