Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Huduma kwa Wateja kutoka
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii, Eunice Chiume (kushoto), akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu Mpango wa Shirika hilo, kukusanya mapato ya shilingi
Bilioni 706.41 kutoka kwenye michango ya wanachama, wakati wa mkutano
uliofanyika leo, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya
Habari, Zamaradi Kawawa. (Picha na Eliphace Marwa-MAELEZO)
SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii katika mwaka huu wa fedha linatarajia kukusanya
mapato ya Tshs. Billion 706.41 kutoka kwenye michango ya wanachama ambao hadi
mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu shirika
lilikua na wanachama 522,763 kwa nchi nzima.
Taarifa
iliyotolewa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya jamii kwa waandishi wa habari
imeeleza kwamba kiasi hicho cha michango kitatokana na uandikishaji wa
wanachama 169,241 wa mpango wa lazima na
wanachama 85,158 wanaojiunga na NSSF kwa njia ya hiari.Katika kipindi
hicho waajiri 3,062 wanatarajia kuandikishwa kwenye Shirika kuungana na waajiri 19,231 wa sasa na kufanya ongezeko la
asilimia 84.07%.
Taarifa pia imeeleza kuwa kiasi cha mafao kitakacholipwa ni
shilingi bilioni 199 kwa wanachama watakaoacha au kustaafu kazi katika mwaka
huu wa fedha.
Katika mwaka huu wa fedha kiasi cha
Tshs.bilioni 5.19 kitalipwa kwa ajili ya mafao ya matibabu kwa wanachama
254,399.
Wakati huo huo katika mwaka huu wa
fedha,shirika linatarajia kuwekeza kiasi cha Tshs. Bilioni 951.4 ukilinganisha
na Tshs bilioni 751.4 ambazo ziliwekezwa katika mwaka wa fedha wa 2012/2013 sawa na ongezeko la aslimia 21.06%.
Shirika
linatarajia pia kukusanya mapato ya
Tshs.bilioni 181.1 kutoka kwenye vitega uchumi ukilinganisha na mapato ya Tshs
bilioni 120.1 zilizokusanywa mwaka jana wa fedha. Maeneo ya uwekezaji ni pamoja na ujenzi wa
daraja la Kigamboni,Dhamana za serikali,mabenki,Ubia(Listed &unlisted
companies) na ujenzi wa nyumba za kuishi na biashara.
Tathmini
ya thamani ya mfuko wa shirika mwaka
jana ilikua Tshs.Trilioni 2.1 na thamani inatarajiwa kuongezeka na kufikia
Tshs.Trilioni 2.6 katika mwaka huu wa fedha ambapo ni sawa na ongezeko la
asilimia 19.23%.
WIKI YA NSSF
Shirika
limeendelea kuadhimisha wiki ya NSSF kila mwaka kwa kushiriki katika shughuli
za kijamii kwa kuendesha michuano ya vyombo vya habari ambapo michezo hiyo
imetimiza mwaka wa 10 tangu ianzishwe mwaka 2004.
Mashindano
hayo ambayo yameanzishwa kwa madhumuni ya kujenga mahusiano kati ya Shirika na
vyombo vya habari mwaka huu yameshirikisha timu 17 za mpira wa miguu na pete ambazo
zilicheza mwezi machi mwaka huu kwa muda wa wiki mbili.
Timu
hizo ni NSSF yenyewe kama mdhamini, TBC, New Habari Corporation, Mwananchi,
Habari Zanzibar, IPP Media,Sahara Communications, Radio Kheri, Free Media, Business
Times, Uhuru/Mzalendo, Global Publishers, Tumaini Media, Changamoto, TSN, Mlimani
Media na Jambo Leo.
Katika
mashindano ya mwaka huu mabingwa kwa upande wa mpira wa miguu ni timu ya Jambo
Leo na mpira wa pete ni Business Times.
TAARIFA
HII IMETOLEWA NA SHIRIKA LA TAIFA LA HIFADHI YA JAMII (NSSF), AUGUST 21, 2013
No comments:
Post a Comment