TANGAZO


Wednesday, August 21, 2013

Profesa Lipumba avinanga Vyombo vya Usalama


Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba (kushoto) na Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Shariff Hamad, wakiingia ukumbini tayari kwa ufunguzi wa kikao cha Baraza Kuu la Uongozi wa chama hicho, Makao Makuu ya CUF, Buguruni Dar es Salaam leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Chama cha CUF, wakiwa katika kikao chao leo jijini Dar es Salaam, wakati Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba alipokifungua.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad, akizungumza kabla ya Mwenyekiti wake, Profesa Lipumba, kukifungua kikao cha Baraza Kuu la Uongozi leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akizungumza wakati akikifungua kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho, Makao Makuu, Buguruni Dar es Salaam leo. Katikati ni Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad na kulia ni Naibu Katibu, Hamad Masoud Hamad. 
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akionesha moja ya nyaraka za utekelezaji wa Bajeti ya nchi kwa Mikoa ya Kusini, wakati akikifungua kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho, Dar es Salaam leo. 

Mwenyekiti wa Chama cha CUF, Profesa Lipumba na Katibu wake Mkuu, Maalim Seif Shariff wakijadili jambo wakati wa ufunguzi wa kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la chama jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Chama cha CUF, wakiwa kwenye kikao chao jijini leo.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Chama cha CUF, wakiwa kwenye kikao chao jijini leo, wakati Mwenyekiti wao, Profesa Lipumba alipokuwa akikifungua.

Na Nyendo Mohamed
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahimu Lipumba amevishutumu vyombo vya usalama kwa kutotumia nguvu nyingi katika kuzuia dawa za kulevya na badala yake kutumia nguvu hizo katika masuala ya kuzuiya maandamano, mikutano na Sheikh Ponda.

Hayo aliyasema Profesa Lipumba Dar es Salaam leo, alipokuwa akifungua kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali yanayoikabili Tanzania.

Alisema kuwa vyombo vya dola vimekuwa vikichangia mtafaruku mkubwa kutokana na kutofanya kazi kwa uweledi na badala yake kuwa ndio chanzo cha kuchochea vurugu nchini.

Lipumba alisema kuwa Vyombo vya dola vineshindwa kushughulikia sula la madawa ya kulevua hadi kusuburi Mwakyembe kulishughulikia ndio wao wajitokeze.

Aliongeza kuwa ameshangazwa sana na kitendo cha Jeshi la Polisi kutumia gharama nyingi katika kuhusu suala la Sheikh Ponda pamoja na Jeshi la Polisi kutumia nguvu kubwa kwa Ponda kama gaidi wa kimataifa.

''Jeshi la polisi limenishangaza sana kwa kuwa wanapoteza gharama nyingi kwa Sheikh Ponda na kupoteza muda wao mwingi kujaza Askari Mkoa wa Morogoro wakati wa kusomea mashtaka utazani Osama ameshuka Tanzania''alisema Lipumba.

Aidha alisema kuwa suala na kipigwa risasi kwa Ponda sio suala la kufurahia kwana jana alikuwa Daud Mwangosya leo Sheikh Ponda kesho anaweza kuwa yeye au yeyote yule.

Hata hivyo alisema kuwa uchumi wa nchi unazidi kushuka huku suala la ajira bado ni ketendawili kwa vijana pamoja na vitendo vya kifisadi vinavyofanywa na badhii ya watendaji Serikalini.

Mabali na hayo Prof Lipumba alisema kuwa rasmi ya katiba bado inahitaji marekebisho mengi ili kupata Khatiba moja itakayo tetea maslahi ya wananchi.

Alifafanua kuwa lengo kikao hicho cha Baraza Kuu ni kuja na agenda Maendeleo ambapo watajadili masula hayo yote ambayo yamekuwa makubwa ambayo yanaweza kuipeleka nchi pabaya.

Alisisitiza kuwa Taifa linahitaji vyombo vya dola ambavyo vinawajibika ipasavyo kwa kufata haki na si kujitolea maamuzi vinginevyo nchi itaelekea pabaya.

No comments:

Post a Comment