TANGAZO


Sunday, August 18, 2013

Mkurugenzi Mtendaji Vodacom Tanzania, Rene Meza, aomba radhi kwa kukosekena mawasiliano kwa muda wa masaa 16

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu kurejea kwa huduma za mawasiliano za kampuni hiyo, zilizopotea kwa saa 16 siku ya Ijumaa, Agosti 16 hadi 17, mwaka huu, baada ya moto kuzuka kwenye mitambo yake ya mawasiliano, pia kurejesha vifurushi mbalimbali vya mawasiliano kwa wateja walionunua huduma hiyo kwa wakati wa kukatika mawasiliano hayo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza, akizungumza na waandishi wa habari, jijini leo, kuhusu kurejea kwa huduma za mawasiliano za kampuni hiyo kama kawaida baada ya kutokupatikana kwa masaa 16, Agosti 16 hadi 17, mwaka huu kutokana na moto kuzuka kwenye mitambo yake yamawasiliano. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, wakati akizungumza kuhusu kurejea kwa huduma za mawasiliano za kampuni pamoja na kuwaomba radhi wateja walioathirika hitilafu hiyo. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano cha kampuni hiyo, Kelvin Twissa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, kuhusu hitilafu iliyotokea kwenye mitambo ya mawasiliano na kurejea kama kawaida kwa huduma za mawasiliano za kampuni hiyo. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano, Kelvin Twissa.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano cha Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika mkutano huo jijini leo. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Rene Meza na Ofisa Mawasiliano Mkuu, Georgia Mutagahywa.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano cha Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa (kushoto), akimuonesha kitu Mkurugenzi Mtendaji, Rene Meza, wakati wa mkutano huo, jijini leo. 
Baadhi ya Maofisa wa Kampuni ya Vodacom Tanzania wakiwa kwenye mkutano huo.

Na Claudia Kayombo
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom, imewahakikishia Watanzania kuwa huduma za mtandao huo ambazo hazikupatikana kwa muda wa masaa 16 kati ya Ijumaa na Jumamosi zimerudi kama mwanzo.

Hali kadhalika imewahakikishia wateja wake walionunua vifurushi mbalimbali vya muda wa maongezi Ijumaa iliyopita, watarejeshewa kesho.

Mkurugenzi Mkuu wa kamapuni hiyo, Rene Meza ameyasema hayo leo, Dar es Salaam wakati akizungumza na wanahabari.

"Mawasiliano ya simu za mkononi ni miundombinu muhimu katika 
maisha yetu ya kila siku, hivyo tunatambua na kuelewa kuwa jinsi ambavyo kukosekana kwa mawasiliano kulivyowaathiri wateja wetu,"alisema Meza.

Alibainisha kuwa hali hiyo haikuwaathiri wateja wa Vodacom pekee bali pia na wa mitandao mingine waliokuwa wanahitaji kuwasiliana na ndugu jamaa na marafiki walioko kwenye mtandao huo.

Alitabaisha kuwa hivi sasa huduma zimerejea kama kawaida na ametoa shukrani kwa wafanyakazi na washirika wao kwa kufanya kila jitihada ili kurejesha huduma za mtandao huo.

Mtandao wa simu za mkononi wa Vodacom haukuwa hewani nchi nzima kwa muda wa saa 15 kuanzia asubuhi ya Ijumaa Agosti 16 hadi 17 mwaka huu hali hiyo ilitokea baada ya mitambo ya kusambazia huduma kushika moto.

No comments:

Post a Comment