TANGAZO


Tuesday, July 16, 2013

Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, NMB kuandaa mafunzo kwa Maofisa Maendeleo




Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa kushirikiana na Benki ya NMB wameandaa mafunzo ya siku mbili kwa Maofisa wa Maendeleo ya Vijana wote nchini kuwafundisha njia za kusimamia masuala yote yanayohusiana na Vijana kwani vijana wanachukua asilimia 68 ya nguvu kazi ya Taifa.

Waziri Dk. Fenella Mukangala
Mheshimiwa Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangala ambaye atakuwa mgeni rasmi atafungua mafunzo hayo yanayotarajiwa kuanza rasmi tarehe 18 Julai, 2013 siku ya Alhamisi saa tatu asubuhi na kumalizika siku ya tarehe 19 Julai, 2013 yatafanyika Uwanja wa Taifa.

Madhumuni makubwa ya mkutano huo ni kuwajengea uwezo Maafisa Maendeleo ya Vijana ili waweze kusimamia, kuratibu na kutathmini vizuri masuala yote ya Maendeleo ya Vijana kote nchini.

Kwa sasa swala kubwa lililopo mbele kuhusiana na Vijana ni Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ambao mwaka huu Serikali imetenga shilingi Bil. 6.1 kwa ajili ya kuwakopesha Vijana na kuwajengea uwezo kupitia mafunzo ya ujasiriamali, uanzishwaji na usimamizi bora wa miradi ya Vijana.

Kwa kuzingatia hilo maswala ya vijana ni maswala mtambuka yanayohusisha sekta zote, hivyo kuna umuhimu wa kutoa mbinu bora kwa wataalamu wa Vijana ili waweze kushirikiana na sekta mbalimbali zinazojihusisha na Vijana kuwasaidia.

Aidha maafisa Vijana licha ya kupata elimu ya jinsi ya kuanzisha, kusimamia na kuendesha miradi endelevu watapata mbinu bora za kuwasaidia Vijana kuanzisha SACCOS za Vijana za Wilaya.

Imetolewa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.


No comments:

Post a Comment