TANGAZO


Saturday, July 6, 2013

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi azindua Ripoti ya Awali ya Utafiti wa ugonjwa wa Kifua Kikuu


Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein 
Ali Mwinyi akihutubia wakati akizindua ripoti hiyo. 
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi (kushoto), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ripoti ya awali ya utafiti wa kwanza wa kutathmini kiwango cha tatizo la Kifua kikuu nchini katika Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam jana. Kulia ni Mtafiti Mwandamizi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Dk. Sayoki Mfinanga na Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania, Rufaro Chatora.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi (kushoto), akionesha ripoti hiyo. Wengine ni viongozi mbalimbali wa wizara hiyo na wawakilishi kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO), Tanzania.
 
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi (kushoto), akionesha ripoti hiyo. Wengine ni viongozi mbalimbali wa wizara hiyo na wawakilishi kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO), Tanzania.
Waziri Mwinyi akimkabidhi cheti mmoja wa watafiti
wa ripoti hiyo.

Waziri Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na 
viongozi mbalimbali baada ya kuzindua rasmi ripoti hiyo.
Wadau na wageni mbalimbali wakifuatilia uzinduzi huo, 
ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam leo.
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye hafla hiyo.

Na Dotto Mwaibale

WAZIRI wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema tatizo la ugonjwa wa kifua kikuu hapa nchini bado ni kubwa hasa katika maeneo ya vijiji.
 
Mwinyi aliyasema hayo wakati akizindua  ripoti ya awali ya utafiti wa kwanza wa kutathmini kiwango cha tatizo la kifua kikuu nchini Tanzania katika ukumbi wa Karimjee Dar es Salaam leo.
 
Alisema ukubwa wa tatizo la kifua kikuu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni wagonjwa kati ya watu wazima 100,000 na kiwango hicho kipo juu zaidi kinapolinganishwa na kile cha 261/100,000 ambacho kilitabiriwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) mwaka 2011.
 
"Ugonjwa huu umeonekana kuwepo kwa wingi zaidi maeneo ya vijijini kuliko mijini na imebainika pia kuwa wanaume wapo kwenye hatari zaidi ya kuugua kifua kikuu kuliko wanawake" alisema Mwinyi.
 
Alisema hayo yamebainika kutokana na utafiti uliofanyika nchi nzima ukihusisha mikoa yote ya Tanzania Bara na miwili kutoka Zanzibar kuanzia Desemba 2011 na kukamilika mwezi Novemba 2012.
 
Alisema mikoa ambayo imeonesha kuathirika zaidi ni Lindi, Mwanza, Shinyanga, Mbeya wakati  Geita zimeonesha kiwango cha juu zaidi na wakati huohuo mikoa ya Pwani, Katavi, Rukwa na Dodoma imeonesha kuwa na viwango vya chini ilikilinganishwa na mingine.
 
Alisema kwa upange wa Zanzibar ugonjwa huo kiwango chake kimeendelea kuwa cha chini.
 
Alisema utafiti huo umeratibiwa na Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu- NIMR chini ya mwongozo wa Shirika la Afya Duniani- WHO, na kuwa matokeo ya utafiti huo yatatoa picha halisi ya hali ya kifua kikuu nchini Tanzania Bara na Zanzibar.
 
"Matokeo ya utafiti huu yatatumika kuwaongoza watunga sera kutengeneza hatua mahsusi za kuboresha udhibiti wake hasa katika nyanja za mwenendo wa kifua kikuu, maambuki ya pamoja ya kifua kikuu na Ukimwi na Kifua Kikuu sugu (MDR-TB) alisema Mwinyi.
 
Alisema serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua umuhimu wa utafiti kuhusu afya hivyo utafiti huo utatoa taarifa muhimu katika kubuni mipango na kufanya maamuzi sahihi katika uboreshaji wa sekta za afya.
 
Aliongeza kuwa kwa kuzingatia hali ya sasa matokeo ya utafiti huo yatachangia vilivyo katika uelewa kwenye kutimiza mikakati ya kitaifa ya kuboresha afya za wananchi.

No comments:

Post a Comment