TANGAZO


Saturday, July 6, 2013

Rais wa Zanzibar, Dk. Shein atembelea Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba jijini Dar es Salaam

Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto), akipatiwa maelezo na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Umoja wa Afrika (UAU), nchini Tanzania, Lee Chang Ki kwenye Viwanja vya vya Maonesho ya Kimataifa vya Biashara 'Sabasaba' Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam leo. Kushoto ni Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (katikati mbele), akipatiwa maelezo na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya kusindika vyakula na majani ya chai, Zanzibar ya ZATEPA FOOD COMPANY LTD, Said S. Hemed (kushoto), alipotembelea banda hilo kwenye Maonesho ya Kimataifa vya Biashara, Viwanja vya Mwalimu Nyerere, 'Sabasaba' Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam leo. Wa pili kushoto ni Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui. 
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (katikati mbele), akiagana na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya kusindika vyakula na majani ya chai, Zanzibar ya ZATEPA FOOD COMPANY LTD, Said S. Hemed (kushoto), mara baada ya kutembelea banda hilo kwenye Maonesho ya Kimataifa vya Biashara, Viwanja vya Mwalimu Nyerere, 'Sabasaba' Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam leo. 
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (katikati mbele), akipatiwa maelezo na Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Ushauri ya MORINGA ya Arusha, Christina Ngoti (kulia), wakati alipotembelea banda hilo, kwenye Maonesho ya Kimataifa vya Biashara, Viwanja vya Mwalimu Nyerere, 'Sabasaba', Dar es Salaam leo. Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Phibele, Christina Mollel.
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) na Waziri wake wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui, wakiangalia chupa zenye viungo (Spices), huku  wakipatiwa maelezo na mke wa Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mama Anna Mkapa (kushoto), wakati walipofika kwenye banda la Wanawake na Maendeleo (WIP) katika sehemu ya Kampuni ya Uzalishaji na Usindikaji wa viungo hivyo ya Zanzibar Spices Producers ya Zanzibar. Kulia ni Mkurugenzi wake, Sharifa M. Mohamed. 
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) na Waziri wake wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui, wakipatiwa maelezo na Mkurugenzi wa Zanzibar VVSABU Spice, Sabra A. Sharif, wakati alipotembelea banda hilo kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara, Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam leo. Kushoto ni mke wa Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mama Anna Mkapa
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto), akiangalia makopo ya vyakula vilivyosindikwa na Kampuni ya Mahayu General Supply, wakati alipotembelea banda la Wanawake na Maendeleo (WIPE), Viwanja vya Kimataifa vya Maonesho ya Biashara vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Rebecca Anyingisye na Mkurugenzi wa Gwassa Enterprises, Kibaha, Stella Gwassa
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) na Waziri wake wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui (kushoto kwake), wakipatiwa maelezo na Mkurugenzi Mwendeshaji wa kundi la Boma Arts and Food Processor, Frida Boma, wakati alipotembelea banda hilo kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara, Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam leo. Kushoto ni mke wa Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mama Anna Mkapa.
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) na Waziri wake wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui (kushoto kwake), wakiangalia vikapu kwenye banda la WIPE, sehemu ya Kampuni ya Lemachi Enterprises, kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara, Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa kampuni hiyo, Mary Chilala na kushoto ni mke wa Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mama Anna Mkapa.
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na Waziri wake wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui (kushoto kwake), wakiangalia paketi ya korosho huku wakipatiwa maelezo na Meneja Mradi wa Kampuni ya Cashew Nut (2005) Ltd, Stephen Emanuel (kulia), kwenye banda la WIPE, katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara, Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam leo. Kushoto ni mke wa Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mama Anna Mkapa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk. Abdalla Kigoda.
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (katikati) na Waziri wake wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui (wa kwanza kulia), wakiangalia mifuko ya kuwekea bidhaa za Kampuni ya SS Bakhresa, wakati alipotembelea banda la Kampuni hiyo katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara, Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam leo. Katikati yao ni Kiongozi wa banda hilo, Abdulkadir Omar na kushoto ni Ofisa Masoko kampuni hiyo, Idd Msoma. 
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (katikati) na Waziri wake wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui (wa kwanza kulia), wakiangalia mifuko ya kuwekea bidhaa za Kampuni ya SS Bakhresa, huku wakimsikiliza Ofisa Masoko kampuni hiyo, Idd Msoma, wakati walipotembelea banda la kampuni hiyo kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara, Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam leo. Katikati yao ni Kiongozi wa banda hilo, Abdulkadir Omar.
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (katikati) na Waziri wake wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui (wa kwanza kulia), wakiangalia kipande cha plastiki cha kutengenezea mifuko ya kuwekea bidhaa za Kampuni ya SS Bakhresa, wakati alipotembelea banda la Kampuni hiyo katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara, Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam leo. Katikati yao, anayewaonesha ni Kiongozi wa banda hilo, Abdulkadir Omar na kushoto ni Ofisa Masoko kampuni hiyo, Idd Msoma. 
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) na Waziri wake wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui (wa pili kulia), wakisikiliza maelezo kutoka kwa Kiongozi wa Banda la Kampuni ya SS Bakhresa, Abdulkadir Omar (kushoto), wakati alipotembelea banda la Kampuni hiyo katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara, Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam leo.
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) na Waziri wake wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui (wa kwanza kushoto), wakisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mifumo cha Kampuni ya Azam Marine, Hussein Abbas, kuhusu usafiri wa meli za kampuni hiyo, wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara, Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment