Kaimu Meneja, Habari na Mawasiliano wa Wakala wa Vipimo (WMA), Irene John, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu kazi na majukumu ya wakala pamoja na uboreshwaji wa mifumo ya ukaguzi. Kulia ni Meneja wa Upimaji, Wakala wa Vipimo, Richard Kadege, Mkurugenzi Msaidizi wa Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Zamaradi Kawawa.
Kaimu Meneja, Habari na Mawasiliano wa Wakala wa Vipimo (WMA), Irene John, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu kazi na majukumu ya wakala pamoja na uboreshwaji wa mifumo ya ukaguzi. Kulia ni Meneja wa Upimaji, Wakala wa Vipimo, Richard Kadege, Mkurugenzi Msaidizi wa Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Zamaradi Kawawa.
Kaimu Meneja, Habari na Mawasiliano wa Wakala wa Vipimo (WMA), Irene John (wa pili kushoto), akizungumza na waandishi wa habari, katika mkutano huo leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Biashara, Deogratias Maneno, Kulia ni Meneja wa Upimaji, Wakala wa Vipimo, Richard Kadege na wapili kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Zamaradi Kawawa.
Meneja wa Upimaji, Wakala wa Vipimo, Richard Kadege, akizungumza na waandishi katika mkutano huo, Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Biashara, Deogratias Maneno, Kaimu Meneja Habari na Mawasiliano, Irene John na Mkurugenzi Msaidizi wa Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Zamaradi Kawawa.
Meneja wa Upimaji, Wakala wa Vipimo, Richard Kadege, akiwaonesha waandishi kipimo cha matenki ya mafuta wakati wa mkutano huo jijini leo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Biashara, Deogratias Maneno, Kaimu Meneja Habari na Mawasiliano, Irene John na Mkurugenzi Msaidizi wa Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Zamaradi Kawawa.
Meneja wa Upimaji, Wakala wa Vipimo, Richard Kadege, akiwaonesha waandishi kifaa cha kutunzia kumbukumbu za upimaji wa magari kinachujulikana kwa jina la kitaalamu cha 'Scanner', wakati wa mkutano huo leo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Biashara, Deogratias Maneno, Kaimu Meneja Habari na Mawasiliano, Irene John na Mkurugenzi Msaidizi wa Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Zamaradi Kawawa.
Baadhi ya waandishi wa habari wakisikiliza maelezo yaliyokuwa yakitolewa na uongozi huo katika mkutano huo jijini leo.
Meneja wa Upimaji, Wakala wa Vipimo, Richard Kadege, akiwaonesha waandishi wa habari namna wafanyabiashara wanavyowapunja wanunuzi wa bidhaa kwa njia ya vipimo vya mizani, wakati taasisi ya Wala wa Vipimo (WMA), walipokuwa wakizungumza nao, Dar es Salaam leo, kuhusu kazi na majukumu ya wakala hiyo pamoja na uboreshawaji wa mifumo ya ukaguzi. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Biashara, Deogratias Maneno, Kaimu Meneja Sehemu ya Habari, Irene John na Mkurugenzi Msaidizi wa Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Zamaradi Kawawa.
Mkurugenzi wa Huduma za Biashara, Deogratias Maneno (kushoto), akifafanua jambo katika mkutano huo leo.
Kaimu Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wakala wa Vipimo Tanzania Irene John akiongea na waandishi wa habari leo, jijini Dar es Salaam kuhusu juhudi zilizofanywa na Serikali kupitia wakala hao kuboresha mifumo ya ukaguzi. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari, Zamaradi Kawawa. (Picha na Elphace Marwa)
Meneja Vipimo toka Wakala wa Vipimo Tanzania Deogratius Kadeghe akiwaonyesha waandishi wa habari moja ya jiwe halisi linalotakiwa kutumika kwa ajili ya vipimo vya bidhaa mbalimbali, katika mkutano uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Idara ya Habari. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Habari, Zamaradi Kawawa. (Picha na Elphace Marwa)
Wakala wa Vipimo ni
mojawapo ya Wakala za Serikali ambayo ilianzishwa tarehe 13
Mei, 2002 kwa Tangazo la Serikali
namba 194 la tarehe 17 Mei, 2002. Lengo la Serikali kuanzia wakala wa Vipimo
ilikuwa ni kuboresha utoaji wa huduma
bora kwa wananchi. Awali, ilikuwa ni Idara ya Serikali chini ya Wizara ya
Viwanda na Biashara.
Ø Jukumu kuu la Wakala wa Vipimo ni kumlinda
mlaji kupitia matumizi ya vipimo sahihi.
Pamoja na huduma
zake nyingi inazotoa Wakala wa Vipimo,
kwa leo tutaueleza umma wa watanzania kuwa tumeboresha mfumo wa ukaguzi wa bidhaa zilizofungashwa. Mfumo huu wa sasa ni wa
ki-electronic ambao umeongeza ufanisi
na kurahisisha kazi za ukaguzi tofauti na hapo
awali ambapo tulikuwa tukitumia njia ya kupima na kukokotoa kwa calculator
njia ambayo ilikuwa ikichukua muda
mrefu siku mbili au zaidi
hadi kutoa uamuzi.
Faida
za kutumia mfumo mpya katika bidhaa zilizofungashwa;
a.
Unarahisisha kazi (simplify work) eg.
zamani tulikuwa tunatumia siku 2 hadi 3 katika ukaguzi wa bidhaa ya aina moja
kwa sasa nusu saa inatosha kukamilisha kazi hiyo.
b.
Utendajika kazi unakuwa wa uhakika na ni wa wazi (measurement results are more
accurate and reliable).
c.
Mteja anaona kazi iliyofanyika ni ya
ufanisi, ya kitaalamu na anapata matokeo ya haraka hivyo anaridhika na huduma anayopatiwa (customer satisfaction).
d.
Mteja anakuwa tayari kulipa ada (create
willingness of customers to pay for service rendered)
Pia, wakala wa Vipimo imeboresha ukaguzi wa malori yabebayo mafuta (Road
Tankers) pamoja na malori yabebayo
mchanga na kokoto,( Sand and Other
Ballast Lories (SBLs) kwa kutumia Kifaa maalum
kinachojulikana kama scanner
tofauti na hapo awali tulipokuwa tukikagua kwa kuangalia nyaraka ( certificates) kwa
macho. Kwa upande wa Malori
yabebayo mafuta tulikuwa tukiangalia chart pamoja na Dip stick
Utaratibu huo ulikuwa ni rahisi kugushiwa na malori ya mchanga
tuliwa tukichora ubavuni kuonesha ujazo
wa lori husika.
Njia
ya sasa ya kutumia scanner ;
a.
Utendaji kazi wake unakuwa ni wa
uhakika na sahihi zaidi katika kubaini sticker
halisi kwa magari yaliyokaguliwa. Hii inatupa uhakika kuwa gari limepimwa kwa mwaka husika.
b.
Kupunguza au kuondoa udanganyifu kwa
wamiliki wa malori hayo.
c.
Mteja kulidhika na ukaguzi huo.
Faida ya Mifumo kwa Serikali:
Itasaidia nchi ya Tanzania kufanya biashara nje ya nchi sababu taratibu za
ufungashaji zitakuwa zimezingatiwa hasa uhakiki wa vipimo.
Faida ya Mifumo kwa Wananchi:
Wananchi
kama walaji wa mwisho wanahakikishiwa
usahihi wa vipimo kwa bidhaa watakazolipia.
Wito kwa watanzania; Tusaidiane kutoa
taarifa pale mnapohisi au kuona wafanyabiashara wasiowaaminifu wanatumia vipimo
pungufu au batili kwa kuwasiliana na ofisi zetu zinazopatikana kila mkoa.
Asanteni
kwa kunisikiliza
No comments:
Post a Comment