TANGAZO


Saturday, July 13, 2013

Taasisi ya Starkey ya Marekani yaanza kuwapatia watu 2000 wenye ulemavu wa masikio vifaa vya kuwasaidia kusikia vizuri

Mwanzilishi wa Taasisi ya kuwasaidia watu wenye usikivu hafifu na wasio sikia ya Starkey, William Austin, akimfanyia uchunguzi wa usikivu kijana Lilian Vincent wa Shule ya Viziwi ya Buguruni, Dar es Salaam kabla ya kufunga vifaa vya kuongeza usikivu, Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk- www.bayana.blogspot.com)
Mwanzilishi wa Taasisi ya kuwasaidia watu wenye usikivu hafifu na wasio sikia ya Starkey, William Austin na mwazilishi mwenzake, mkewe Tani Austin, wakimfanyia majaribio ya usikivu kijana Lilian Vincent wa Shule ya Viziwi ya Buguruni, Dar es Salaam wakati wakimfunga kifaa cha kuongeza usikivu, Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam leo.
Mwanzilishi wa Taasisi ya kuwasaidia watu wenye usikivu hafifu na wasio sikia ya Starkey, William Austin na mwazilishi mwenza, mkewe Tani Austin, wakimfunga kifaa cha kuongeza usikivu kijana Lilian Vincent wa Shule ya Viziwi ya Buguruni, Dar es Salaam Hoteli ya Serena, jijini leo.
Mwanzilishi wa Taasisi ya kuwasaidia watu wenye usikivu hafifu na wasio sikia ya Starkey, William Austin akimfunga kifaa hicho kijana Lilian Vincent wa Shule ya Viziwi ya Buguruni. Kushoto ni mwazilishi mwenza, mkewe Tani Austin.
Mwanzilishi wa Taasisi ya kuwasaidia watu wenye usikivu hafifu na wasio sikia ya Starkey, William Austin akimfunga kifaa hicho kijana Lilian Vincent wa Shule ya Viziwi ya Buguruni. Kushoto ni mwazilishi mwenza, mkewe Tani Austin.
Mwanzilishi wa Taasisi ya kuwasaidia watu wenye usikivu hafifu na wasio sikia ya Starkey, William Austin akimvalisha kijana Lilian Vincent wa Shule ya Viziwi ya Buguruni, medali baada ya kufanikiwa kurudisha usikivu wake. Kushoto ni mwazilishi mwenza, mkewe Tani Austin.

Kijana akifanyiwa majaribio wakati akifungwa kifaa hicho cha usikivu.
Waanzilishi hao, wakimfanyia majaribio wakati wakimfunga kifaa hicho cha usikivu kijana huyu.
Wakimfunga kifaa hicho mara baada ya kufanikiwa katika majaribio ya kifaa hicho cha usikivu.

 Baadhi ya vijana wakisubiri kupatiwa huduma hiyo, Hoteli ya Serena, Dar es Salaam leo.


Kijana akisafisha masikio kabla ya kufungwa kifaa cha kuongeza usikivu na kumwezesha asiyesikia kupata usikivu.
 Vijana wakijiorodhesha kupatiwa huduma hiyo hotelini hapo leo.
 Baadhi ya vijana wakiwa tayari baada ya kufungwa vifaa hivyo vya usikivu.

Mwanzilishi wa Taasisi ya kuwasaidia watu wenye usikivu hafifu na wasio sikia ya Starkey, William Austin na mwazilishi mwenzake, mkewe Tani Austin, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchi wanaosaidia kufanikisha huduma hiyo, hotelini hapo. Wa pili kushoto ni Teddy Mapunda. 

Na Lorietha Laurence-MAELEZO-Dar es salaam
ZAIDI ya wakazi 2000 wa jiji la Dar es Salaam wenye matatizo ya kusikia  wanatarajiwa kupata huduma ya vifaa vitakavyosaidia kusikia vizuri.

Huduma hiyo, inatarajiwa kutolewa na Mfuko wa Starkey Hearing  kwa muda wa siku nne katika Hoteli ya Serena.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, jijini Dar es salaam Mwanzilishi wa  Mfuko   huo William Austin amesema kuwa sikio ni kiungo muhimu kwa binadamu ndio maana mfuko wake umeamua kuwasaidia watu mbalimbali duniani ili wasione kama wametengwa.

"Mimi nimeoma muda wangu mwingi  katika kuwasaidia watu wasio na uwezo katika kuwapatia vifaa ambavyo kiasi kikubwa vitawaunganisha na watu wengine na hivyo kushiriki katika mijadala ya kuwaletea maendeleo yao na jamii yao" alisema Austin.

Alisema kuwa umati ulijitokeza unaonyesha kuwa wananchi wengi wanasumbuliwa na matatizo ya masikio na hivyo wanahitaji huduma ya vifaa ili waweze kuwasiliana na wenzao wasio na matatizo.

Mpango huo umeanzia hapa jijini Dar es salaam ambapo kwa wastani wanatarajia kutoa huduma kwa watu 600 kila siku kwa muda wa siku nne.

No comments:

Post a Comment