TANGAZO


Tuesday, July 16, 2013

Serikali yatangaza msimu mpya wa ununuzi wa mazao ya kilimo

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari, Zamaradi Kawawa (katikati) akifungua mkutano wa waandishi wa habari na Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika katika ukumbi wa Idara ya Habari leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Msemaji wa Wizara hiyo, Richard Kasuga na kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Chakula, Karim Mtambo.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini wakiwa kazini katika kuhakikisha wananchi wanapata taarifa kutoka kwa wawasilishaji wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika katika ukumbi wa Idara ya Habari leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Msaidizi Mtafiti Mazao wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Dk. Hussein Mansoor (kushoto) akifafanua kwa waandishi wa habari kuhusu mkakati wa Wizara hiyo kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula juu ya ununuzi wa nafaka kwa kuzingatia gharama za uzalishaji pamoja na bei ya soko katika eneo la ununuzi. Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Biashara wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula, Mikalu Mapunda.
Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Chakula kutoka Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Karim Mtambo (kulia) akifafanua jambo kwa vyombo vya habari nchini juu ya Uanzishwaji wa Msimu Mpya wa Ununuzi wa Nafaka. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari, Zamaradi Kawawa.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula, Charles Walwa(kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari juu ya mkakati wa Wakala hao katika ununuzi wa nafaka kwa kuzingatia gharama za uzalishaji pamoja na bei ya soko katika eneo la ununuzi, katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya Habari leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Msemaji wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Richard Kasuga. (Picha zote na Hassan Silayo-Maelezo)

KUANZA KWA MSIMU MPYA WA UNUNUZI WA NAFAKA
Tathminiya awali ya uzalishaji wa mazao ya chakula katika msimu wa 2012/2013 na upatikanaji wa Chakula kwa mwaka wa 2013/2014 inayoendelea inaonesha kuwa hali ya uzalishaji wa mazao ya chakula unaridhisha katika mikoa 19 kati ya mikoa yote 25. Upatikanaji wa vyakula sokoni unaridhisha katika mikoa yote 25 na bei zinaendelea kushuka kadri uvunaji unavyoendelea.
Kama ilivyo kawaida kwa kila mwaka, Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (National Food Reserve Agency-NFRA) imeshaanza kununua nafaka kwa ajili ya kuongeza hifadhi ya chakula yaTaifa.  Wakala imeanza kufanya ununuzi huo kupitia kanda zake saba za Kipawa, Arusha, Shinyanga, Dodoma, Makambako, Songea na Sumbawanga kuanzia mwezi Julai, 2013. Mazao yatakayo nunuliwa ni mahindi na mtama katika maeneo yenye ziada ya uzalishaji, hususan vijijini, lengo likiwa ni kununua tani 200,000. Aidha, Wakala utaingia kwenye soko la mazao yanayokusudiwa kama mnunuzi mwingine.
Jumla ya vituo 58 vitatumika kununua mazao katika kanda saba za Wakala kama ifuatavyo (Idadi ya vituo kwenye mabano): Sumbawanga (17), Songea (20), Makambako (8), Dodoma (4), Shinyanga (4) Arusha (3) na Kipawa (2). Aidha jumla ya vyama vya Ushirika 52 vimeonyesha nia ya kuuza nafaka kwa Wakala. Vituo vitakavyotumika kwa ununuzi zimeoneshwa katika Kiambatisho Na. 1.
Nafaka zinazouzwa kwa Wakala zinatakiwa kukidhi vigezo vya ubora kama vile kukaushwa vizuri, kutokuwa na takataka, zisiwe na punje zilizovunjika, punje zisiwe zimeliwa na wadudu, punje zisiwezimeoza, zisiwembovu au zisiwe na rangi tofauti. Wizara inasisitiza kuwa wakulima wahakikishe wanauza mahindi yenye ubora unaotakiwa ambayo hayajaathiriwa na ugonjwa wa mahindi ìMaize Lethal Necrotic (MLND).î
Wizara kupitia NFRA utanunua nafaka kwa kuzingatia gharama za uzalishaji pamoja na bei ya soko katika eneo la ununuzi. Pale ambapo bei ya soko hairudishi gharama za uzalishaji kwa mkulima, Wakala utanunua nafaka kwa bei inayorudisha gharama ya mkulima.
Wizara pi a inaelekeza wanunuaji wote wa mazao kuhakikisha wanatumia vipimo sahihi vya uzito wakati wa zoezi la ununuzi.
Njia za ununuzi zitakazotumika msimu huu ni kama zifuatazo:-
ï Kutumia vituo vya ununuzi ambavyo vitanunua mahindi moja kwa moja kutoka kwa wakulima
ï Kuingia katika mikataba na vikundi na vyama vya wakulima kama vile SACCOS na AMCOS kwa lengo la kuimarisha vyama vya Ushirika nchini kwa kuvipatia soko la uhakika.
ï Kuteua na kuingia mikataba na mawakala wa ununuzi
ï Kutumia zabuni ya wazi ya umma hasa katika maeneo yenye uzalishaji mdogo ya mikoaya Dodoma, Shinyanga na Arusha.
Wakala huifadhi chakula kwa lengo la kuongeza akiba ya chakula ya Taifa hivyo kuongeza uwezo wa Serikali kuwahudumia wananchi wake wakati kunapokuwa na uhaba wa chakula. Wakulima wanashauriwa kujiwekea akiba ya kutosha ya chakula katika kaya na kuuza kwa Wakala ziada inayopatikana kwa kuwa bei inayotoa ni nzuri na ya uhakika na kwa lengo la kusaidia nchi yetu kuwa na uhakika wa chakula. Uhakika wa chakula ni usalama wa Taifa hivyo kwa pamoja tunaweza kukabiliana na janga la njaa ili pasiwepo Mtanzania atakaye kufa kwa njaa.
Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula - National Food Reserve Agency (NFRA) ni Taasisi ya Umma iliyo chini ya Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika. Wakala ulianzishwa chini ya sheria ya Wakala wa  Serikali Na. 30 ya mwaka 1997 kwa madhumuni ya kuhakikisha usalama wa chakula nchini ili kukabiliana na upungufu wa chakula. Majukumu  mahususi ya NFRA ni pamoja na kununua, kuhifadhi na kuzungusha (re-cycling) akiba ya chakula na kutoa chakula kwa waathirika waliokumbwa na upungufu wa chakula kwa maelekezo ya Ofisi ya Waziri Mkuu, kitengo cha Maafa.Ununuzi hufanyika kila mwaka katika maeneo yaliyozalisha  ziada kwa lengo la kuongeza akiba ya chakula ya taifa.
Imetolewa na:
KATIBU MKUU
WIZARA YA KILIMO CHAKULA NA USHIRIKA
Kiambatisho Na. 1:   VITUO VYA UNUNUZI KATIKA KANDA ZA WAKALA
KANDA WILAYA KITUO CHA UNUNUZI MALENGO YA
UNUNUZI  (MAHINDI) MALENGO YA UNUNUZI MTAMA
SUMBAWANGA Sumbawanga Manispaa Mazwi 11,000
SUMBAWANGA Sumbawanga Manispaa Bohari 5,500
SUMBAWANGA Sumbawanga Kaengesa 1,500
SUMBAWANGA Kalambo Matai 3,500
SUMBAWANGA Kalambo Mkombo 2,500
SUMBAWANGA Sumbawanga Mtowisa 2,500
SUMBAWANGA Nkasi Ntalamila 2,000
SUMBAWANGA Kalambo Mwimbi 2,500
SUMBAWANGA Kalambo Katazi 1,500
SUMBAWANGA Sumbawanga Laela 4,500
SUMBAWANGA Sumbawanga Sandurula 1,500
SUMBAWANGA Nkasi Swaila 1,000
SUMBAWANGA Nkasi Namanyere 3,000
SUMBAWANGA Nkasi Mtenga 2,500
SUMBAWANGA Nkasi Kasu 2,000
SUMBAWANGA Mlele Majimoto 1,500
SUMBAWANGA Mlele Kibaoni 1,500
Jumla ndogo 50,000 0
SONGEA Songea mjini Ruhuwiko 7,000
SONGEA Songea mjini Mwanamonga 600
SONGEA Songea vijijini Nakahuga 600
SONGEA Songea vijijini Mkenda 10,000
SONGEA Songea vijijini Madaba 1,500
SONGEA Songea vijijini Mgazini 4,000
SONGEA Songea vijijini Lusonga 1,800
SONGEA Songea vijijini Litisha 1,500
SONGEA Songea vijijini Magagula 3,000
SONGEA Songea vijijini Muungano zomba 800
SONGEA Namtumbo Hanga 500
SONGEA Namtumbo Mkongo 1,300
SONGEA Namtumbo Namabengo 1,200
SONGEA Namtumbo mjini Namtumbo 800
   WILAYA KITUO CHA UNUNUZI MALENGO YA UNUNUZI  (MAHINDI) MALENGO YA UNUNUZI (MTAMA)
SONGEA Namtumbo Kitanda 1,800
SONGEA Mbinga Kindimba juu 1,600
SONGEA Mbinga Tingi 1,800
SONGEA Mbinga Mbinga 2,000
SONGEA Mbinga Matiri 3,000
SONGEA Mbinga Kigonsera 3,200
SONGEA Songea SACCOS 2,000
Jumla ndogo       50,000.00 0
MAKAMBAKO Makambako Makambako 12,000
MAKAMBAKO Ludewa Mlangali 4,000
MAKAMBAKO Ludewa Shaurimoyo 4,000
MAKAMBAKO Wanging'ombe Igwachanya 1,500
MAKAMBAKO Ileje Ileje 6,000
MAKAMBAKO Ludewa Mawengi 1,000
MAKAMBAKO Ludewa Ludewa 4,000
MAKAMBAKO Mbozi Mbozi 7,500
Jumla ndogo 40,000 0
DODOMA Dodoma Dodoma 5,000 3,000
DODOMA Kongwa Matongoro 2,000
DODOMA Kiteto Engusero 3,000
DODOMA Manyoni Manyoni 2,000
Jumla ndogo 10,000 5000
ARUSHA Arusha Arusha 9,000
ARUSHA Babati Babati 7,000
ARUSHA Babati Gallapo 4,000
Jumla  ndogo 20,000 0
SHINYANGA Tabora Nzega-Bukene 5,000
SHINYANGA Shinyanga Shinyanga mjini 2,500
SHINYANGA Musoma Musoma 2,500
SHINYANGA Kigoma Kibondo 5,000
Jumla ndogo 10,000 5000
KIPAWA Morogoro Morogoro 5,000
KIPAWA Handeni Handeni 5,000
Jumla ndogo 10,000 0
 
Jumla kuu     190,000.00        10,000.00

No comments:

Post a Comment