Mwishoni mwa wiki NMB, ilifadhili mkutano wa makampuni na
taasisi ambazo zimepewa dhamana ya uchimbaji na usambazaji wa mafuta na gesi
nchini. Mkutano huo ulifanyika katika Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam kwa siku mbili ukiambatana na maonyesho ya biashara kutoka makampuni
tofauti nchini Tanzania.
Dhumuni kubwa la mkutano huu lilikuwa ni kutengeneza mahusiano
baina ya wafanya biashara na kujadili jinsi ambavyo huduma zitolewazo na
makampuni na taasisi zilizopewa dhamana ya uchimbaji na usambazaji wa mafuta na
gesi nchini zinavyoweza kuisaidia jamii husika.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Miamala kwa Taasisi NMB, Gerald
Kamugisha akielezea jinsi NMB inavyoweza kusaidia makampuni na taasisi mbali
mbali zinazosambaza mafuta na gesi nchini Tanzania.
Kamishina wa
Nishati na masuala ya Petroli, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Hosea
Mbise,akimkabidhi cheti Mkuu wa kitengo cha huduma za miamala kwa
taasisi NMB, Gerald kamugisha kwa udhamini ambao NMB umetoa ili
kufanikisha mkutano huo.
Meneja ukuzaji wa
biashara NMB, Masato Wasira akiwaelezea baadhi ya washiriki wa mkutano huo juu
ya huduma zitolewazo na benki ya NMB.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wakisikiliza kwa
makini.
No comments:
Post a Comment