TANGAZO


Tuesday, July 9, 2013

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) chatoa taarifa ya Uwekezaji


Meneja Huduma wa Kituo cha Uwaekezaji Tanzania (TIC), Revocatus Arbogast, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu mafanikio ya uwekezaji. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Pendo Gondwe na kushoto ni 

 

Picture 251
Meneja Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Pendo Gondwe akiwaelezea waandishi wa habari juu ya mafanikio ya kuhamasisha uwekezaji kwa wawekezaji wa ndani kwa kipindi cha kuanzia Januari 2012 mpaka Disemba 2012  katika ukumbi wa Idara ya Habari, Maelezo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Zamaradi Kawawa na kulia ni Meneja Huduma Revocatus Arbogast. (Picha zote na Eliphace Marwa)

KITUO cha Uwekezaji  Tanzania TIC kinapenda kutoa taarifa kwa Umma kuhusu mafanikio ya kuhamasisha uwekezaji kwa wawekezaji wa ndani kwa kipindi cha kuanzia Januari 2012 mpaka Decemba 2012.

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) ni moja Taasisi ya Serikali ilianzishwa chini ya Sheria ya Uwekezaji Tanzania, Namba 26 ya mwaka 1997 kwa kuendeleza, kuratibu na kuwezesha uwekezaji katika Tanzania. Kama sehemu ya jukumu letu, TIC ina jukumu la kuhamasisha uwekezaji na masuala yanayohusiana na Uwekezaji kwa Watanzania ili Uwekezaji uweze kuwa na manufaa kwa Watanzania kwa ujumla.
Katika kipindi cha mwaka Januari 2012 mpaka Desemba Watanzania wameweza kutambua umuhimu wa kuwekeza na wameweza kuchangamkia fursa katika sekta mbalimbali. Katika kipindi hicho zaidi ya miradi 869 iliweza kusajiliwa miradi ambayo inategemea kuzalisha kazi zaidi ya 174,412 yenye thamani ya mitaji ya dola 11,420 milioni. Namba ya miradi hii ni kubwa kuwahi kusajiliwa na Kituo.
Miradi ya watanzanzia iliweza kuongoza kwa kwa TIC kusajili miradi 469 ya wazawa ambayo ni asilimia 54% ya miradi yote iliyoweza kusajiliwa.
Sekta tano zilizoongoza katika kusajiliwa ni sekta ya Utalii, Usafirishaji, Uzalishaji viwandani , majengo ya biashara na kilimo. Sekta ya utalii iliongoza kwa kusajili miradi 144, Usafirishaji miradi 92, Uzalishaji viwandaji miradi 86, majengo ya biashara miradi 78 na kilimo miradi 28.
Katika usajili wa miradi hiyo wawekezaji wa nje waliweza kusajiri miradi 205 ambayo ni asilimia 23.5, kiwango ambacho ni chini ya nusu ya kiwango cha usajili wa miradi ya wawekezaji wa ndani. Miradi ya Ubia kati ya wageni na watanzania ilikuwa ni 195 ambayo ni asilimia 22.5.
TIC katika jitihada zake za kuongeza faida za uwekezaji katika uchumi wa Tanzania pia walifanya shughuli kuu ikiwa ni pamoja na kuwawezesha wawekezaji kupata vibali vyote vinavyohitajika chini ya One Stop Shop na utoaji wa huduma kwa wawekezaji aftercare.

No comments:

Post a Comment