TANGAZO


Tuesday, July 23, 2013

Benki ya Barclays yatoa msaada wa sh.milioni 120 kwa mafunzo ya Vijana


Meneja  wa Mawasiliano na Huduma za Jamii wa Benki ya Barclays Bi.Tunu Kavishe  akiongea na waandishi wa habari kuhusu msaada wa Sh.milioni 120 uliotolewa na benki  hiyo kwa shirika lisilo la kiserikali la Nkwamira kwa ajili ya mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana 100. Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Nkwamira, Bi. Noreen Mazalla na kushoto ni Bi. Alice Mwilu kutoka shirika hilo. (Picha na Lorietha Laurence –Maelezo)
Meneja  wa Mawasiliano na Huduma za Jamii wa Benki ya Barclays  Bi.Tunu Kavishe (kushoto), akikabidhi hundi yenye thamani ya Sh. milioni 120 kwa Mkurugenzi wa Shirika la Nkwamira Bi. Noreen Mazalla (kulia), wanaoshuhudia katika ni wafanyakazi wa Nkwamira, Alice Mwilu na Davis Davis. (Picha na Lorietha Laurence –Maelezo)
 Meneja  wa Mawasiliano na Huduma za Jamii wa Benki ya Barclays Bi.Tunu Kavishe  akiongea na waandishi wa habari kuhusu msaada wa Sh.milioni 120 uliotolewa na benki  hiyo kwa shirika lisilo la kiserikali la Nkwamira kwa ajili ya mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana 100. Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Nkwamira, Bi. Noreen Mazalla na kushoto ni Bi. Alice Mwilu kutoka shirika hilo. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

 Meneja  wa Mawasiliano na Huduma za Jamii wa Benki ya Barclays Bi.Tunu Kavishe  akiongea na waandishi wa habari kuhusu msaada wa Sh.milioni 120 uliotolewa na benki  hiyo kwa shirika lisilo la kiserikali la Nkwamira kwa ajili ya mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana 100. Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Nkwamira, Bi. Noreen Mazalla na kushoto ni Bi. Alice Mwilu kutoka shirika hilo.Meneja  wa Mawasiliano na Huduma za Jamii wa Benki ya Barclays Bi.Tunu Kavishe  akiongea na waandishi wa habari kuhusu msaada wa Sh.milioni 120 uliotolewa na benki  hiyo kwa shirika lisilo la kiserikali Nkwamira kwa ajili ya mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana 100,Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Nkwamira Bi. Noreen Mazalla na kushoto ni Bi.Alice Mwilu kutoka shirika hilo. 
Meneja  wa Mawasiliano na Huduma za Jamii wa Benki ya Barclays Bi.Tunu Kavishe  akiongea na waandishi wa habari kuhusu msaada wa Sh.milioni 120 uliotolewa na benki  hiyo kwa shirika lisilo la kiserikali la Nkwamira kwa ajili ya mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana 100. Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Nkwamira, Bi. Noreen Mazalla na kushoto ni Bi. Alice Mwilu kutoka shirika hilo. 

Na Jannifer Chamila-Maelezo
BENKI ya Barclays  imekabidhi hundi ya Sh. milioni 120 kwa  shirika lisilo la kiserikali lijulikanalo kama Nkwamira kwa ajili ya mafunzo ya ujasiriamali kwa  vijana 100  walioshindwa kuendelea na masomo kwa sababu mbalimbali kutoka mikoa ya Dar Es Salaam na Morogoro.

Meneja wa Mawasiliano na Huduma za Jamii wa benki hiyo, Bi.Tunu Kavishe  akiongea na waandishi wa habari leo, jijini Dar es Salaam amesema kuwa mkakati huo utawapa vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 35 fursa ya kupata nafasi ya kujiendeleza na kujiajiri.

“Mpango huu utawashirikisha vijana 60 kwa mkoa wa Dar Es Salaam na vijana 40 kwa mkoa wa Morogoro  kupitia mitihani mbalimbali  ambayo itaendeshwa  na wataalamu wa biashara na fedha  kutoka vyuo vikuu vya Tanzania ambapo watawachuja vijana hao na kupatikana washindi wawili”.alisema Bi.Tunu

Aliongeza kuwa mpango huu umeanza kwa mikoa ya Dar es Salaam na Morogoro na baadaye kufuatia na mikoa mingine nchini ili kuweza kuwafikia vijana wengi zaidi na kusaidia Serikali katika juhudi za kuwakomboa vijana.

Naye Mkurugenzi wa shirika hilo, Bi. Noreen Mazalla alisema” Tunashukuru kwa msaada waliotupatia Benki ya Barclays na sisi tunaahidi kuufanyia kazi kwa kuwanufaisha vijana ili waweze kujikwamua kimaisha na kulijenga Taifa letu”.

Pia alitoa wito kwa vijana walioshindwa kuendelea na masomo ya sekondari baada ya kumaliza elimu ya msingi na wale  walioshindwa  elimu ya sekondari  kidato cha nne na sita  kufika Mlimani City kwa ajili ya kujiandikisha na kuweza kupata nafasi ya kushiriki katika mafunzo hayo.

Benki ya Barclays imekuwa ikifanya juhudi za kuwakomboa vijana ili waweze kujiajiri na wakati mwingine kuwaajiri katika Benki yao kwa kupitia programu  ya  kuwapa mafunzo wahitimu wa vyuo (graduate recruitment trainee).

No comments:

Post a Comment