TANGAZO


Sunday, June 23, 2013

Vodacom yashindanisha watoto DarLive, Yawataka wanawake vijijini kutumia vema mikopo ya Mwei kujikwamua kiuchumi

Baadhi ya watoto wakiwa tayari kushindana katika mbio za Vodacom Cheka Nao zilizofanyika Dar Live, Mbagala siku ya kifamilia iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania kwaajili ya Promosheni ya Cheka Nao, inayowawezesha wateja kupiga simu kwa bei nafuu kwenda mitandao yote nchini na kujishindia shilingi milioni 2 kila mmoja kwa mwezi, ili kujiunga na kufaidika na ofa  piga *149*01#.

Baadhi ya watoto wakiwa tayari kushindana katika mbio za Vodacom Cheka Nao zilizofanyika Dar Live, Mbagala siku ya kifamilia iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania kwaajili ya Promosheni ya Cheka Nao inayowawezesha wateja kupiga simu kwa bei nafuu kwenda mitandao yote nchini na kujishindia shilingi milioni 2 kila mmoja kwa mwezi,ili kujiunga na kufaidika na ofa  piga *149*01#.


Ofisa wa Vodacom Tanzania Alfani Mdachi(katikati)akimwandikisha Mustafa Mustafa mkazi wa Mbagala ili kumpatia kadi ya simu tayari kwa matumizi halali zoezi hilo lilifanyika wakati wa kampeni ya Cheka Nao inayowawezesha wateja wa kampuni hiyo kupiga simu kwa bei nafuu kwenda mitandao yote nchini na kujishindia shilingi milioni 2 kwa mwezi,ili kujiunga na kufaidika nayo piga *149*01#.Anaeshuhudia ni Meneja wa kanda ya Mbagala Idd Mawe.

Ofisa wa Vodacom Tanzania bi.Rehema William(alieketi)akimwelezea jambo mkazi wa mbagala Dar es Salaam,wakati Promosheni ya Cheka Nao iliyofanyika mbagala hapo jana inayowawezesha wateja wa kampuni hiyo kupiga simu kwa bei nafuu kwa mitandao yote nchini na kujishindia shilingi milioni 2 kwa mwezi,ili kujiunga na kufaidika nayo piga *149*01#.

Bi.Tumu Saidi ambae ni mkazi wa Mbagala,Dar es Salaam akimsikiliza Ofisa wa Vodacom Tanzania jinsi anavyomfafanunua faida za kujiunga na Promosheni ya Cheka Nao inayowawezesha wateja wa kampuni hiyo kupiga simu kwa bei nafuu kwa mitandao yote nchini na kujishindia shilingi milioni 2 kwa mwezi,ili kujiunga na kufaidika nayo piga *149*01#,Wanaoshuhudia kushoto ni Meneja wa kanda ya Mbagala Idd Mawe na kulia ni Meneja Uhusiano wa Kampuni hiyo Bw.Matina Nkurlu.


Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Bw.Matina Nkurlu(kulia)akimwelezea Bi.Tumu Saidi ambae ni mkazi wa Mbagala,Dar es Salaam manufaa na faida za kujiunga na Promosheni ya Cheka Nao inayowawezesha wateja wa kampuni hiyo kupiga simu kwa bei nafuu kwenda mtandao wowote na kujishindia shilingi milioni 2 kwa mwezi,ili kujiunga na kufaidika nayo piga *149*01#,Wanaoshuhudia kushoto ni Meneja wa kanda ya Mbagala Idd Mawe.


MWANAMKE akipewa fursa  anaweza hutenda makubwa katika kulisaidia Taifa kujiendeleza kiuchumi kupitia nyanja mbalimbali.

Hayo yalisemwa na mtendaji wa kijiji cha Madaba Bi. Gloria Wendelin Komba baada ya yeye pamoja na akina mama wengine 284 kutoka vijiji mbalimbali vilivyopo Wilaya ya Songea Vijijini kupokea  mikopo ili kukuza mitaji ya biashara zao.

Kina mama hao kutoka vijiji 17 wilayani Songea Vijijini walifaidika na mikopo yenye thamani ya zaidi ya Tsh. 17m/- kutoka kwenye mradi MWEI wa mfuko wa Vodacom wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation na kuahidi kutumia mikopo hiyo kukuza mitaji ya biashara zao na hatimae kujikwamua wao na familia zao kiuchumi.

Katika hafla hiyo ya kukabidhiwa mikopo yao, mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Songea Bw.Joseph Mkirikiti aliwaasa kina mama hao waitumie mikopo hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa ili waweze rudisha mikopo kwa wakati muafaka ili kuwawezesha kina mama wengine wapate mikop[o na hatimae kuinua uchumi wa wilaya hiyo kwa pamoja.

“Lazima kila mmoja aone ni fursa ya kipekee kwenu na iwe chanzo cha kufungua milango kwa wanyonge wengi walioko mijini na vijijini  kuwezeshwa kujikwamua kiuchumi na kuleta maendelea katika vijiji,tarafa wilaya na hatimae taifa zima.” Aliongeza.

Mkuu wa Wilaya hiyo alisema kuwa yeye na uongozi mzima wa Wilaya yake, watahakikisha kuwa program hii ya MWEI kutoka Vodacom Foundation itakuwa endelevu na hakutakuwa na upendeleo, rushwa au kitu chochote kitakachokwamisha mpango huu.

Mbali na mikopo hiyo, kina mama hao zaidi ya 300, walipata fursa ya kukumbushwa kuhusu miiko ya ujasiriamali ili ziwasaidie katika kukuza mitaji yao na hatimae kukuza biashara.

Meneja wa mradi wa MWEI, Mwamvua Mlangwa, alisema nia ya Vodacom Foundation ni kuinua kipato cha mwanamke mwenye kipato cha chini kupitia mikopo hiyo kwani mwanamke ni uti wa mgongo wa uchumi wa familia.

Amesema kwa kushirikiana na serikali za vijiji, wilaya na mikoa husika, Vodacom Foundation imeanzisha  mchakato huu wa kuwawezesha kina mama na utaleta maana pale tu wale kina mama waliochukua mikopo wataitumia kuinua kipato chao na kurejesha mikopo hiyo kwa wakati muafaka ili kuwawezesha na wengine pia kupata fursa hiyo.

“Mikopo itolewayo na MWEI ni ile isiyo na riba ili kumwezesha mkopaji kuitumia kupata faida na kukuza mtaji wake na pia kurahisisha urejeshaji  kwa urahisi na unafuu. Urejeshaji huu hauna usumbufu kwani kiongozi wa kikundi hutumia huduma ya M-Pesa iliyo salama na inayoaminika katika marejesho” aliongeza Mlangwa.

M-Pesa Women Empowerment Intiative- MWEI ni mradi ulioanzishwa kuwasaidia kina mama wenye kujishughulisha na biashara ndogo ndogo kuongeza mitaji ya biashara zao na hatimae kujikwamua kiuchumi. Hii ni mikopo ya kwanza kutolewa kwa akina mama wa Songea na vijiji vyake tangu kuanza mwaka wa fedha 2013/14.

No comments:

Post a Comment