Katibu Mkuu wa Chama cha Wachezaji Mpira Tanzania (SPUTANZA), Said George, akiongea huku akiwa na baadhi ya viongozi wenzake wa chama hicho wakati wa utoaji wa tuzo za wachezaji Bora wa Chama hicho kwa mwaka 2013, ukumbi wa Diamond Jubilee usiku wa kuamkia leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-bayana.blogspot.com)
Makamu wa Pili wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Athuman Nyamlani, akizungumza wakati alipokuwa akifungua utoaji wa tuzo ya Mwanasoka bora wa SPUTANZA, ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo. Kulia ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Said George.
Baadhi ya vingozi wa Kishen Enterprises, moja ya wadhamini wa tuzo hizo, wakiwa katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo, ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
Wasanii wa Sky Light Band wakitumbuiza katika utoaji wa tuzo hizo, ukumbini humo.
Mkurugenzi wa Kishen Eterprises, wauzaji wa pikipiki za Lifan, ambao ni moja ya wadhamini wa tuzo hizo, Rajen Solank (kushoto), akimkabidhi Meck Mexime tuzo ya kocha bora wa msimu.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah, akiongea kabla ya kumtaja mchezaji boara anayechipukia, ambaye alikuwa Salum Abubakar tuzo ya Sputanza, baada ya kuwashinda wenzake kadhaa katika katagoria hiyo.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah, akimkabidhi mchezaji boara anayechipukia, Salum Abubakar tuzo ya Sputanza, baada ya kuwashinda wenzake kadhaa katika katagoria hiyo.
Mwenyekiti wa SPUTANZA, Mussa Kissoky, akimkabidhi tuzo ya golika bora Kocha wa Mtwibwa, Mecky Mexime.
Mkurugenzi wa Kishen Eterprises, wauzaji wa pikipiki za Lifan, ambao ni moja ya wadhamini wa tuzo hizo, Rajen Solank (kulia), akizungumza kwa ajili ya kumtambulisha kwa mashabiki wa Mwakilishi wa Kampuni ya Lifan, Nasikiwa Benya (kushoto), wakati wa hafla hiyo. Katikati ni Katibu Mkuu wa SPUTANZA, Said George.
Makamu wa Pili wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Athuman Nyamlani, akipanda kuijaribu pikipiki ya kike, aliyozawadiwa mke wa Rais, Mama Salma Kikwete na kukabidhiwa yeye na Mkurugenzi Kishen Enterprises, katika hafla hiyo usikuwa wa kuamkia leo, ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Athuman Nyamlani, akikabidhiwa zawadi na Mmoja wa wanafamilia ya Pepsi, ambao ni moja ya wafadhili wa tuzo hizo, Fadi El-Khalil.
Wanafamilia ya Pepsi, Fadi El-Khalil (kulia) na Meneja Mkuu wa Uhasibu Taifa wa Kampuni ya Pepsi, ambao ni moja ya wafadhili wa tuzo hizo, Bhank Patwa, wakifungua bahasha yenye jina la mchezaji bora wa jumla SPUTANA, ambapo Amri Kiemba wa Simba aliibuka kinara.
Meneja Mkuu wa Uhasibu Taifa wa Kampuni ya Pepsi, ambao ni moja ya wafadhili wa tuzo hizo, Bhank Patwa (kushoto), akiwa na mwanafamilia ya Pepsi, Fadi El-Khalil (katikati), akimkabidhi Mohamed Bhinda kwa niaba ya mchezaji bora wa jumla wa SPUTANA, Amri Kiemba wa Simba ambaye hakuwepo katika hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment