TANGAZO


Tuesday, May 7, 2013

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Shamsi Vuai Nahodha, aufungua mkutano wa viongozi wa Dini wa Kujadili amani mkoani Dar es Salaam



Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Mecki Sadiki, 

akizunguza katika mkutano aliouandaa kwa viongozi wa dini 

za Kiisalamu na Kikristo pamoja na Kamati za Ulinzi na 

Usalama, mkaoni Dar es Salaam leo, kabla ya kumkaribisha 

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Shamsi 

Vuai Nahodha(kulia kwake), kuufungua mkutano huo wa 

siku mbili.



Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Shamsi 

Vuai Nahodha, akizungumza wakati akiufungua mkutano wa 

Mkuu wa Mkoa na Kamati za Ulinzi na Usalama pamoja na 

viongozi wa dini, kujadili mustakabali wa hali ya amani 

mkoani Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Mkoa, 

Saidi Sadiki. 


Baadhi ya viongozi wa dini za Kiislamu na Kikristo, wakimsikiliza Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Shamsi Vuai Nahodha, wakati akiufungua mkutano wao na Mkuu wa Mkoa pamoja na Kamati za Ulinzi na Usalama, kujadili mustakabali wa hali ya amani mkoani Dar es Salaam leo.
Viongozi wa dini za Kiislamu na Kikristo, wakimsikiliza Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Shamsi Vuai Nahodha, wakati akiufungua mkutano huo wa kujadili mustakabali wa hali ya amani mkoani Dar es Salaam leo.

Baadhi ya viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wakiwa katika mkutano huo wa kujadili mustakabali wa hali ya amani mkoani Dar es Salaam leo, wakimsikiliza Waziri Shamsi Vuai, wakati akiufugua leo mchana.


Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Shamsi 

Vuai Nahodha, akiufungua mkutano ulioandaliwa na Mkuu 

wa Mkoa kwa Kamati za Ulinzi na Usalama pamoja na 

viongozi wa dini, kujadili mustakabali wa hali ya amani 

mkoani Dar es Salaam leo.

Viongozi wa dini za Kiislamu na Kikristo, wakiwa katika mkutano huo, wakati ukifunguliwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Shamsi Vuai Nahodha, Dar es Salaam leo.

Baadhi ya viongozi wa dini za Kiislamu na Kikristo, wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Shamsi Vuai Nahodha, wakati akiufungua mkutano wao jijini leo.

Baadhi ya viongozi mbalimbali wa dini za Kiislamu na Kikristo pamoja na wa Ulinzi na Usalama, wakimsikiliza Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Shamsi Vuai Nahodha.

Viongozi wa dini za Kiislamu na Kikristo, wakiwa kwenye  mkutano wao.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki, 

akimpongeza Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa 

(JKT), Shamsi Vuai Nahodha, mara baada ya kuufungua 

mkutano huo. 



Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Shamsi 

Vuai Nahodha, akipongezwa na Askofu wa Kanisa la Inland 

Charch, Dayosisi ya Pwani Charles Salala, mara baada ya 

kuufungua mkutano huo. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Dar 

es Salaam, Saidi Sadiki.


Askofu wa Kanisa la Inland Charch, Dayosisi ya Pwani 

Charles Salala, akitoa neno la shukurani, mara baada ya 

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Shamsi 

Vuai Nahodha, kuufungua mkutano huo leo.




Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Shamsi 

Vuai Nahodha, akisindikizwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es 

Salaam, Saidi Sadiki, wakati akiondoka mara baada ya 

kuufungua mkutano huo.



Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Shamsi 

Vuai Nahodha, akisalimiana na Sheikh Ali Basaleh, wakati 

aliondoka kwenye mkutano huo.


Na Claudia Kayombo
SERIKALI imesema itakuwa na ukali zaidi ya simba dhidi ya mtu yeyote atakayetoa kauli za kukashifu dini nyingine hapa nchini.

Pia imetoa mwito kwa waumini wa madhehebu ya dini za Kiislamu na Kikristo nchini, kufikisha kero zao kwa Waziri wa Nchi Ofisi Rais Uhusiano na Uratibu, Stephen Wasira ili zifanyiwe kazi.


Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha aliyasema hayo leo, wakati akifungua kongamano la siku mbili la viongozi wa madhehebu ya Dini za Kikristo na Kiislamu pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani Dar es Salaam wa kujadili mustakabali wa hali ya amani mkoani humo.


"Katika hili Serikali inawajibu wa kuchukua hatua za kisheria dhidi ya watu wanaokashifu imani za wengine. Itakuwa kama jabali na ukali zaidi ya simba.


Na Serikali itakuwa na upole kama sungura kwa watii,"alisema Waziri huyo wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.


Aliongeza kuwa viongozi wa dini wana nguvu kubwa katika kusuluhisha migogoro katika jamii kuliko wa siasa.


Alibainisha kuwa kiongozi wa siasa anaweza kutumia wiki nzima (siku saba) kujaribu kutafuta suluhu ya mgogoro lakini wa dini  anatumia saa 1 tu.


Hata hivyo Waziri Nahodha alionesha mashaka kuwa huenda kukua kwa tatizo la udini nchini kunasababishwa na baadhi ya viongozi wa dini kuonekana katika macho ya watu kuwa wanahubiri msamaha huku ndani wanawaambia lipizeni kisasi.


Alisema masuala ya uchochezi wa kidini ama ukabila ni mabaya sana kwani mfano wa mataifa yaliyoingia katika machafuko kutokana na uchochezi wa kidini na kikabila ni Rwanda, Lebanon, Afrika ya Kati na Ivory Coast.


Akifafanua alisema Lebanon ambayo Mji wake Mkuu Beirut, lilikuwa taifa lenye watu wengi lakini baada ya kuingia katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe imebaki na magofu yenye ukiwa.


Alisema kwa sasa Tanzania inapita katika kipindi kigumu zaidi ya muda wote wa Uhuru wa miaka 50 ya nchi hiyo.


Alibainisha kuwa ni vyema sasa viongozi wa dini wakawa na maeneo maalum ya kuzungumza mambo ya msingi ya kidini na waamini wao kuliko kukaa viwanjani na kutoa kashfa dhidi ya imani nyingine.


Akitoa neno la shukrani Askofu Charles Salalah, wa Afrika Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Pwani, alisema anamshukuru Mungu kwa kuwakutanisha wao viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini hizo lakini pia kwa maneno ya hekima aliyoyatoa Waziri Nahodha.


Pia alisema ni wajibu wa viongozi wa dini na Watanzania kutafakari kilichowafikisha walipo kisha kutafuta suluhu ya nini kifanyike kuirudisha nchi katika hali ya amani na utulivu.


Hata hivyo alisema midhara ya kidini si mibaya miongoni mwa imani zote bali kinachochafua ni maneno kashfa dhidi ya madhehebu mengine yanayotolewa na baadhi ya wahubiri ambayo huzaa chuki miongoni mwa waumini wa madhehebu tofauti.


Naye Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam, Alhad Salum alisema baada ya mkutano huo ni matumaini yake kuwa kila mshiriki atakwenda kuhubiri kuvumiliana kwani amani ikitoweka hakuna atakayebaki salama.

No comments:

Post a Comment