TANGAZO


Tuesday, May 7, 2013

Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi duniani Kitaifa kufanyika mkoani Rukwa, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Mwinyi kuwa mgeni rasmi

Rais wa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA), Paul Magesa akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu maadhimisho ya Siku ya Wauguzi duniani itakayoadhimishwa Kitaifa nchini, mkoani Rukwa Mei 12, mwaka huu, ambapo mgeni rasmi wa maadhimisho hayo, atakuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi. Kulia ni Ofisa Habari wa Idara ya Habari (Maelezo), Eliphace Marwa. (Picha zote na Kassim Mbarouk) 



Waandhishi wa habari, wakimsikiliza Rais wa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA), Paul Magesa wakati alipokuwa akizungumza nao, Dar es Salaam leo, kuhusu maadhimisho ya Siku ya Wauguzi duniani itakayoadhimishwa Kitaifa nchini mkoani Rukwa, Mei 12, mwaka huu.


Rais wa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA), Paul Magesa akizungumza na waandishi wa habari (kulia), Dar es Salaam leo, kuhusu maadhimisho ya Siku ya Wauguzi duniani itakayoadhimishwa Kitaifa nchini mkoani Rukwa, Mei 12, mwaka huu.

Waandhishi wa habari, wakiandika habari zilizokuwa zikitolewa na  Rais wa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA), Paul Magesa wakati alipokuwa akizungumza nao, Dar es Salaam leo, kuhusu maadhimisho ya Siku ya Wauguzi duniani itakayoadhimishwa Kitaifa nchini, mkoani Rukwa Mei 12, mwaka huu.

Na: Eliphace Marwa – Maelezo
07-05-2013
CHAMA cha Wauguzi Tanzania kimesema kuwa vifo vya mama  wajawazito  pamoja na watoto vimepungua sana nchini kutokana na kuboreshwa na kufikishwa kwa huduma muhimu  kwa walengwa.
Kauli hiyo imetolewa na Rais wa chama hicho, Paulo Magesa wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam juu ya Maadhimisho ya Siku ya Waaguzi Duniani  yatakayofanyika Mei 12 mwaka huu.
Magesa alisema  maadhimisho hayo yanayotarajiwa kufanyika kitaifa mkoani Rukwa, yatakuwa na kauli mbiu inayosema kuwa “Kuziba pengo kufikia Malengo ya Milenia  namba 6,5,4”.
Alisema  kuwa malengo hayo  ya millennia yanalenga kuzuia vifo vya kinamama wajawazito wakati wa kujifungua, kuzuia vifo vya watoto wenye umri chini ya miaka mitano na kuzuia maambukizi ya Virusi Virusi UKimwi(VVU) kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
 “Pamoja na changamoto nyingi tunazokutana nazo wauguzi bado tunajitahidi kwa kadri ya uwezo wetu kuhakikisha  na hii imeleta mafanikio makubwa  kwani”, alisema Magesa.
 Alifafanua kuwa  pamoja na changamoto nyingi wanazokutana nazo wauguzi nchini,  bado wanajitahidi kwa kadri ya uwezo wao kuhakikisha  huduma bora zinawafikia walengwa na hilo limeleta mafanikio makubwa.
Katika kuzuia na kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto nchini chini ya mpango wa Milenia,Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imelenga kuhamasisha akina mama kutumia njia salama za uzazi wa mpango na kuhakikisha wanajifungulia kwenye  vituo vya  kutolea huduma za mama na mtoto.
Katika maadhimisho hayo kutakuwa na maonesho kuanzia Mei 10 hadi Mei  12, kuonesha shughuli mbalimbali za kitaaluma wanazozifanya wauguzi ikiwa ni pamoja na kutoa huduma mbalimbali za kiafya kama huduma ya mama na mtoto, huduma za kupima VVU na ushauri nasaha.
Chama cha wauguzi Tanzania (TANNA) ni chama kinachowawakilisha wauguzi na wakunga wote Tanzania bara na Katika maadhimisho hayo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Hussein Mwinyi.

No comments:

Post a Comment