TANGAZO


Monday, April 29, 2013

Waziri Kombani afungua mkutano kuhusu mchango wa Utumishi wa Umma katika utekelezaji wa mpango wa maendeleo wa miaka mitano, jijini Dar es Salaam

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani, akifuatana na Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, HAB Mkwizu, Mwakilishi mkazi wa Kanda ya Afrika Mashariki, jijini Nairobi wa Taasisi ya HANS SEIDEL ya Ujerumani, Markus Baldus (nyuma) na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya CAFRAD, Dk. Simon Mamos, wakati akiwasili kuufungua mkutano kuhusu mchango wa Utumishi wa Umma katika utekelezaji wa mpango wa maendeleo wa miaka mitano, Dar es Salaam leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk)


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani (katikati), mara baada ya kuwasili ukumbi wa Kivukoni, Hoteli ya Serena kuufungua mkutano huo. Wa pili kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, HAB Mkwizu, Mwakilishi mkazi wa Kanda ya Afrika Mashariki, jijini Nairobi wa Taasisi ya HANS SEIDEL ya Ujerumani, Markus Baldus (kushoto) na wa pili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya CAFRAD, Dk. Simon Mamos.


Mwakilishi mkazi wa Kanda ya Afrika Mashariki, jijini Nairobi wa Taasisi ya HANS SEIDEL ya Ujerumani, Markus Baldus, akizungumza kuelezea kazi na shughuli mbalimbali zinazofanywa  na taasisi yake, kabla ya Waziri Kombani kuufungua mkutano huo.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya CAFRAD, Dk. Simon Mamos, akizungumza kuielezea kazi ya taasisi yake hiyo, kabla ya Waziri Kombani kuufungua mkutano huo.

Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, HAB Mkwizu, akizungumza pamoja na mambo mengine, kuhusu matumaini yake kwa washiriki wa mkutano huo, kwamba watayapa kipaumbele mafunzo na utekelezaji wake ili kufanikisha malengo ya mkutano huo, pia Kaimu Katibu Mkuu huyo, alitumia nafasi hiyo, kumkaribisha Waziri Kombani kuufungua rasmi mkutano huo.

Baadhi ya washiriki wa mkutano huo, ambao ni Manaibu Katibu Wakuu kutoka Wizara mbalimbali, Watendaji Wakuu wa Wizara zinazojitegemea (MDAs), Washirika wa maendeleo, Wawakilishi wa Vyuo Vikuu na sekta binafsi, wakisikiliza hotuba ya Kaimu Katibu Mkuu, HAB Mkwizu, wakati akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri Kombani.

Washiriki wa mkutano huo, wakisikiliza hotuba hiyo kwa makini kabla ya kufunguliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani leo.


Baadhi ya washiriki wa mkutano huo, ulioandaliwa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, wakiwemo Viongozi na Watendaji wa Wizara mbalimbali pamoja na wadau wa maendeleo, wakiandika maelezo ya hotuba zilizokuwa zikitolewa na watendaji wa ofisi hiyo.

Washiriki wa mkutano huo, wakiwemo baadhi ya Wakurugenzi wa Ofisi hiyo, Manaibu Katibu Wakuu wa Wizara pamoja na taasisi za sekta binafsi, wakifuatilia hotuba iliyokuwa ikitolewa na Waziri Kombani, wakati alipokuwa akiufungua mkutano huo jijini leo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani, akizungumza wakati alipokuwa akiufungua mkutano kuhusu mchango wa Utumishi wa Umma katika utekelezaji wa mpango wa maendeleo wa miaka mitano, Dar es Salaam leo.

Washiriki wakifuatilia hotuba ya Waziri Kombani katika ufunguzi huo leo.


Wajumbe wa mkutano huo wa siku mbili, wakiwa katika ufunguzi leo huo, ukumbi wa Hoteli ya Serena (Movenpick), jijini Dar es Salaam leo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani, akizungumza wakati akiufungua mkutano huo, kuhusu mchango wa Utumishi wa Umma katika utekelezaji wa mpango wa maendeleo wa miaka mitano, Dar es Salaam leo. Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, HAB Mkwizu na Mwakilishi mkazi wa Kanda ya Afrika Mashariki, jijini Nairobi wa Taasisi ya HANS SEIDEL ya Ujerumani, Markus Baldus.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani, akizungumza na waandishi wa habari, wakati alipokuwa akifafanua masuala mbalimbali kuhusu mkutano huo, mara baada ya kuufungua.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani (katikati waliokaa), akiwa na wajumbe wa mkutano huo, mara baada ya kuufungua, Hoteli ya Serena (Movenpick), Dar es Salaam leo. Wa pili kushoto waliokaa ni Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, HAB Mkwizu, wa kwanza kulia ni Mwakilishi mkazi wa Kanda ya Afrika Mashariki, jijini Nairobi wa Taasisi ya HANS SEIDEL ya Ujerumani, Markus Baldus na wa pili ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya CAFRAD, Dk. Simon Mamos.

No comments:

Post a Comment