TANGAZO


Monday, April 29, 2013

Mwanafunzi wa Chuo cha Ualimu Kigoma, aibuka Milionea wa Vodacom

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa (katikati), akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, mara baada ya kumpata mshindi wa droo ya mwisho ya 'MAHELA,' Valelian Nickodemus(22) wa Mkoa wa Kigoma, aliyejishindia sh. milioni 100. Kushoto ni Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha nchini, Mrisho Mlau na kulia ni Meneja wa Huduma za Ziada wa Vodacom Tanzania,  Benjamin Michael. (Picha zote na mpigapicha wetu)

Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa (katikati), akiongea na mshindi wa droo ya mwishi ya 'MAHELA,' Valelian Nickodemus (22) wa Mkoa wa Kigoma aliyejishindia sh. milioni 100. Kushoto ni Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha nchini, Mrisho Milau na kulia ni Meneja wa Huduma za Ziada wa Vodacom Tanzania, Benjamin Michael.


Kutoka kushoto, Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha nchini, 

Mrisho Milau, Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, 

Matina Nkurlu pamoja na Meneja wa Huduma za Ziada wa 

kampuni hiyo, Benjamin Michael, wakichezesha droo ya 

mwisho ya "MAHELA," ambapo Valelian Nickodemus (22), 

Mwanafunzi wa Chuo cha Uwalimu, mkoani Kigoma alijishindia 

kitita cha sh. milioni 100, kupitia promosheni hiyo.


Na mwandishi wetu

HATIMAYE Mshindi wa Milioni 100 wa Promosheni ya 

Vodacom Mahela amepatikana ikishuhudia Mwanafunzi chuo cha 

Ualimu cha Mkoani Kigoma Bw.Valelian Nickodemus(22) 

akiibuka  mshindi kupitia droo kubwa iliyochezeshwa  leo 

Jumatatu.

Mshindi huyo amepatikana miongoni mwa mamilioni ya washiriki 

walioshiriki kucheza katika promosheni hiyo, Katika mahojiano 

yaliyofanyika kwa njia ya simu Mshindi huyo ameishukuru 

Kampuni ya Vodacom kwa kumuwezesha kushinda kiasi hiko 

kwani hayakuwa mategemeo yake katika maisha yake.


"Watu wengi hawakuwa wanaamini kuwa Promosheni hizi ni za 

kweli, Sikuwa na pesa ya kucheza moja kwa moja katika 

Promosheni hii ila nilipotumiwa pesa ya matumizi na mzee 

niliamua kuweka na kushiriki katika Promosheni hii, Hakika 

nimefurahi sana na ninawashukuru Vodacom, alisema 

Nickodemus.


Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano 

wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa amewapongeza Wateja wa 

mtandao huo kwa kushiriki katika promosheni hiyo na 

kumpongeza kwa upekee mshindi wa Promosheni hiyo na 

kujinasibu kuwa anajivunia mafanikio ambayo Promosheni hiyo 

imeyapata kwa kufanikiwa kubadili maisha ya mamia ya 

Watanzania.


"Sisi kama Vodacom tumefurahi kwa kumpata mshindi wetu wa 

mwisho ambaye ameibuka kidedea kati ya Mamilioni ya 

Watanzania lazima tukiri kuwa ni bahati kubwa na tunatoa pongezi 

za kipekee kwa mshindi wetu, alisema Twissa na kuongeza kuwa

"Zaidi ya yote tunajivunia kwa upekee kabisa namna ambavyo 

promosheni hii imebadilisha mamia ya maisha ya Watanzania, 

Tumepata washindi kutoka katika Nyanja mbalimbali wakiwemo 

wakulima, wafanya biashara ndogondogo wanafunzi pamoja na 

wastaafu wengi ambao nao wameendelea kuboresha maisha yao," 

alisema.


Tangu Promosheni ya MAHELA kuzinduliwa tarehe 24 Mwezi wa 

kwanza na washindi 333 wamepatikana  na kushuhudia kiasi cha 

Shilingi milioni 480 zikitolewa hadi sasa.

No comments:

Post a Comment