TANGAZO


Monday, April 29, 2013

Ofisa Mtendaji Mkuu wa PEPSI atembelea Tanzania

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya SBC, watengenezaji wa soda za Pepsi, akiongea na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo nchini, Ziad El Khalil kiwandani jijini Dar es Salaam leo.



Katibu Mkuu Viwanda na Biashara, Joyce Mapunjo, akizungumza na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Pepsi Mashariki ya Kati, Asia na Afrika, Saad Abdul-Latif.

Na Mwandishi Wetu


Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya vinywaji baridi ya PEPSI 

kwa Bara la Asia, Mashariki ya Kati na Afrika, Bw. Saad 

Abdul Latif, hivi karibuni alifanya ziara nchini Tanzania ikiwa ni 

sehemu ya ziara ya kuzitembelea nchi za ukanda wa Afrika 

Mashariki (Kenya, Tanzania na Uganda).


Katika ziara hiyo, Bw. Latif, aliambatana na Rais wa Kampuni 

hiyo ya PEPSI kwa bara la Asia, Mashariki ya Kati na Afrika, 

Bw. Sanjeev Chadha, ambapo waliweza kukutana na kufanya 

mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, 

Biashara na Masoko, Bi. Joyce Mapunjo.


“Ni furaha kubwa kuwa hapa nchini Tanzania. Kubwa 

ninaomba muwe na uhaikika ya kwamba Kampuni ya PEPSI, i
medhamiria kuhakikisha kwamba wateja wake wanafurahia 

bidhaa zenye ubora wa kimataifa katika bei nafuu zilizo za 

kirafiki,” alisema Bw. Latif.


Akizungumza kwa niaba ya Serikali, Bi. Mapunjo aliishukuru 

Kampuni hiyo ya PEPSI kutokana na ahadi yake iliyojiwekea 

ya kusaidia katika suala zima la maendeleo ya kiuchumi hasa 

katika juhudi zake za kuboresha viwanda, masoko, 

miundombinu na usambazaji.


“Kampuni ya PEPSI nchini (SBC Tanzania) inazalisha na 

kutengeneza nafasi za ajira nchini Tanzania,” aliongeza Bi. 

Mapunjo.


Hivi karibuni Kampuni ya SBC imeanzisha kiwanda cha 

kisasa cha PEPSI katika jiji la Nairobi, ambapo matokeo 

yake yamekuwa mazuri naya kutia moyo kutoka kwa wateja. 

SBC si tu inatoa chaguo la ziada kwa wateja wake kwenye 

vinywaji vyake, lakini pia inatoa thamani ya ziada kwa fedha.


Vinywaji hivi vya PEPSI venye ujazo wa 350 ML kwenye glasi 

kinauzwa bei ya kawaida ambayo ni sawa na bei ya chupa 

yenye ujazo wa 300 ML. Ni pamoja na Pepsi, Mirinda, 

Mountain Dew na aina tofauti za Evervess.


Kampuni ya SBC Tanzania, ni kampuni pekee inayozalisha 

bidhaa mbalimbali za PEPSI nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment