Miraji Mdigo wa Simba SC, akiuondoa mpira miguuni mwa Kipre Tchetche wa Azam FC katika mchezo huo.
Kipre Tchetche wa Azam FC, akijaribu kumpiga chenga Shomari Kapombe wa Simba SC katika mchezo huo.
Mchezaji Kipre Tchetche wa Azam FC na Miraji Mdigo wa Simba wakiwania kuudhibiti mpira wa juu, wakati timu zao zilipopambana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana. Timu hizo zilitoka suluhu kwa kufungana mabao 2-2.

Kipre Tchetche wa Azam FC, akiubeba mpira kuupeleka kati huku akipongezwa na wenzake baada ya kuifungia goli timu yake hiyo kwa njia ya penalti katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Simba SC, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana.
Ubao wa matangazo ukionesha Simba SC 2 na Azam FC 1 baada ya Kipre Tchetche kuifungia timu yake kwa njia ya penalti.
Kipre Tchetche wa Azam FC akiukimbilia mpira baada ya Miraji Mdigo wa Simba kudondoka chini wakati wa mchezo huo jana.
Nassoro Said 'Cholo' wa Simba akiruka juu kuupiga mpira kichwa, katika kuondosha hatari langoni mwa timu hiyo jana.
Shomari Kapombe wa Simba akiutoa mpira miguuni mwa Kipre Tchetche wa Azam FC katika mtanange huo, ulioishia kwa kufungana mabao 2-2.
No comments:
Post a Comment