'Inna Lillahi wa inna Ilaihi raji'un'

Habari tulioipata sasa hivi kuwa Msanii Mkongwe na Muziki wa Taraab wa Kikundi cha Taraab cha 'The East African Melody,' Haji Mohammed, Kijikuu cha Siti Bint Saad, amefariki dunia wakati akipelekwa katika Hospitali ya Muhimbili baada ya kuzidiwa na mapigo ya moyo, asubuhi ya leo, majira ya saa nne.
Marehemu alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya kisukari kwa muda mrefu na presha, mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa mchana huu na boti ya Kampuni ya Azam Marine saa 9.45 jioni kwa ajili ya maziko yatakayofanyika Mjini Zanzibar.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Melody, Hashim Salum amesema amezungumza na marehemu asubuhi na kamwambia anakwenda hospitali kuonanana Daktari wake,, na kushtuka kupata habari ya Msiba huo majira ya saa 4,asubuhi.
Marehemu Haji Mohammed ameacha watoto watatu. 'Mungu alaze pahala pema Peponi roho ya marehemu, 'Amani'.
No comments:
Post a Comment