TANGAZO


Monday, April 15, 2013

Kinana, Nape waivamia Ulanga



Mbunge wa Ulanga Magharibi, Dk. Haji Mponda (kulia), akijadiliana jambo na Katibu wa NEC-CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakati wa ziara ya kikazi ya kuimarisha chama, Jimbo la Ualnga Magharibi leo.

Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulrahman Kinana akiwaongoza baadhi ya viongozi wa chama hicho, kutoka kwenye pantoni ya Mv .Umoja kutoka Ifakara kwenda wilaya ya Ulanga kuimarisha uhai wa chama hicho .

Nape Nnauye akiingia kwenye mtumbwi jana eneo la Kivukoni, Kata ya Minepa, wilayani Ulanga, akiwa katika ziara ya uimarisha uhai chama hicho.


Nape akihutubia mkutano wa ndani wa chama hicho, leo katika Kata ya Mtimbila, Ulanga Magharibi.

Kinana akivishwa skafu baada ya kupokelewa katika Kata ya Minepa alipowasili kuhamasisha uhai wa chama katika Jimbo la Ulanga Mashariki leo.

Baadhi ya wafuasi wa CCM, wakishangilia wakati Katibu wa NEC-CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubiamkutano wa ndani katika Kata ya Mtimbila, Jmbo la 
Ulanga Magharibi.
Katibu wa NEC-CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye  akiwaongoza baadhi ya viongozi wa chama hicho kutoka kwenye pantoni ya Mv. Umoja kutoka Ifakara kwenda Wilaya ya Ulanga, kuimarisha uhai wa chama hicho leo asubuhi.

Nape Nnauye, akivuka kwa kutumia mtumbwi.
Kinana akizungumza na Mmasai, mwanachama wa CCM katika Kata ya Minepa Ulanga leo. (Picha zote na Richard Mwaikenda)

No comments:

Post a Comment