Waziri wa ulinzi wa Ufaransa , Jean-Yves Le Drian, amesema wiki
tatu za mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa kiisilamu, zimewaacha wapiganaji hao
wakiwa wametawanyika wasijue la kufanya.
Bwana Le Drien alisema wapiganaji hao wametoroka Mali wakati wengine
wakitorokea maeneo ya milimani baada ya kushindwa vita.Aidha Bw Le Drian ameunga mkono pendekezo la kutuma majeshi ya umoja wa mataifa nchini Mali na pia kuitikia wito wa majeshi hayo kuunga mkono juhudi za Ufaransa.
Ikiwa mpango kama huu utaidhinishwa, wanajeshi wa Ufaransa pamoja na wale wa mataifa ya Afrika ambayo yanahudumu nchini Mali yatashirikishwa
No comments:
Post a Comment