TANGAZO


Wednesday, January 2, 2013

Wanajeshi wa kigeni watumwa Afrika ya Kati

 

Wanajeshi wa waasi katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati
Jeshi la eneo la Afrika FOMAC katika Jamhuri ya ya Afrika ya kati kwa sasa linaimarishwa na vikosi vya mataifa jirani wakijumuisha wanajeshi elfu mia moja na ishirini kutoka Jamuhuri ya Demokrasi ya Congo DRC.
 
Kamanda wa FOMAC, amesema kuwa wanjeshi hao wataenda kuulinda mji wa Damara, dhidi ya waasi wanokaribia jiji kuu la Bangii.
Msemaji wa waasi hao jijini Paris, anasema ameliambia shirika la Reuters kuwa wamesitisha kidogo safari yao na huenda wakajianda kwa mazungumzo ili kupata suluhu ya kisiasa.

Serikali ya Gabon imesema kuwa itatuma kikosi cha wanajeshi 120, huku serikali ya Cameroon vile vile ikitarajiwa kutuma kiasi kama hicho.

Hili ndilo tishio kubwa zaidi kuwahi kukumba serikali ya rais Francois Bozize, tangu alipotwaa uongozi wa taifa hilo kupitia mapinduzi ya serikali mwaka wa 2003.

Waasi wao wa Seleka, walianza kampeini dhidi ya serikali ya mwezi uliopita na tarayi wameteka miji kadhaa ikiwemo mji wa Bria ulio na utajiri mkubwa wa madini la Almasi.

No comments:

Post a Comment