Takriban watu ishirini wamefariki kwenye ajali mbaya ya
barabarani nchini Kenya, baada ya gari moja ya abiria maarufu kama matatu,
kukosa mwelekeo na kutumbukia ndani ya chimbo la mawe.
Ripoti zinasema watu wengine saba wako katika hali mahututi.
Gari hilo ambalo linaruhusiwa kubeba abiria kumi na wanne pekee inasemekana
kubeba zaidi ya abiria 28.
Idara ya polisi nchini humo imeanzisha uchunguzi kufuatia ajali hiyo.
Afisa mkuu wa polisi katika eneo hilo amesema, maafisa wa polisi watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa itabainika kuwa gari hilo lilipita katika kituo chochote cha ukaguzi na hakiku kamatwa kwa kubeba abiria kupita kiasi.
No comments:
Post a Comment